Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka  Wakurugenzi na
Wakuu wa Wilaya za Dodoma kukamilisha miradi yote kwa wakati  kabla ya kukamilika mwaka wa fedha wa 2022/2023 ambao utafikia tamati ifikapo Juni 30, 2023.

Senyamule ametoa maagizo hayo leo Mei 25, 2023 alipofanya kikao kazi na viongozi wa Halmshauri za Wilaya na Mji za Mkoa wa Dodoma katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi yake.

“Tumebakiwa na takribani mwezi mmoja wa kukamilisha miradi yote kwa muda uliowekwa tunatakiwa kufanya haraka na kwa weledi kabla ya Juni 30, kwakuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatafuta fedha kwa kasi kwahiyo na sisi aliotuteua kumsaidia tunatakiwa tufanye kazi kwa nguvu ili kumuunga mkono.

“Lazima tufanye ubunifu ili majengo ya miradi tuliyopatiwa fedha yakamilike kwa wakati na niwasisitize muwalipe mafundi fedha zao kwa wakati kwasababu ukishamlipa fundi atafanya kazi kwa weledi, vilevile tununue vifaa kwa wakati ili kuondoa ucheleweshaji wa namna yoyote ili iwe ikiwa ni pamoja na kuwakwamisha kuendelea na kazi zao kwa
mujibu wa mpango kazi uliopo” amesema Senyamule.
 
Aidha amewaasa viongozi hao wa Wilaya kufanya uchambuzi wa vyanzo vyote ambavyo havikukusanya mapato na kuvitafutia namna nzuri ya kukusanya mapato na amebainisha kuwa Mkoa umekusanya mapato kwa asilimia 76 huku asilimia 24 pekee zikisali. Senyamule amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji na Wilaya.