Na Dotto Kwilasa, JAMHURI MEDIA, Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Tundu Lissu amefika katika kituo kikuu cha Polisi Dodoma kuona gari alilokuwemo ndani yake wakati akishambuliwa September 7,2017 Jijini hapa eneo la Area D.

Ikiwa imepita miaka sita tangu ashambuliwe,Tundu Lissu amesema hiyo ni mara yake ya kwanza kuliona gari hilo na kueleza kuwa lina matundu ya risasi 30 ambayo yote yalimlenga mtu mmoja ambaye ni yeye.

Akizungumza leo Mei 9,2023 na Waandishi wa habari kwenye eneo ambao gari hilo limeegeshwa amesema kwa mara ya kwanza tangu alipo shambuliwa ameliona gari lake kwani tangu ashambuliwe hakuwahi kuliona.

Aidha ameliomba Jeshi hilo kuendelea kumsaka aliye husika na shambulio dhidi yake na kumshughulikia kwa mujibu wa Sheria. 

“Nilifanya mawasiliano na uongozi wa Jeshi la Polisi Dodoma nashukuru wameniwezesha kuliona,nimehesabu matundu ya risasi yapo 30,imenifikirisha sana kwamba risasi zile zilielekezwa Kwa mtu mmoja ni unyama wa hali ya juu,”amesema

Ameongeza kuwa mara baada ya kukamilisha nyaraka muhimu atachukua gari hilo ili maisha mengine yaendelee.

Kuhusu maneno yaliyopo kwamba Polisi walizuia gari hilo Lissu amesema huo ni uvumi na kwamba hakuna siku amewahi kukatazwa na Jeshi hilo kuona gari lake.

“Kuchukua hii gari sio kwamba naondoa au nafuta kesi , kulingana na Sheria za Tanzania kesi za aina hii zinahesabika kama jinai,kesi hízi huwa mali ya Jamhuri,Mimi sina uwezo wa kuamua kesi ifanyike au isifanyike Mimi natumika kama shahidi tu,”amesisitiza

Mbali na hayo Mwanasiasa hiyo amekanusha tuhuma za  kukataa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwake na kusema hajawahi kufanya hivyo kwani anaelewa hilo ni kosa la jinai na halikubaliki kisheria. 

“Puuzeni maneno ya kijingajinga ,siku zote Nimekuwa nikitoa ushirikiano kwa Polisi na hadi Sasa natamani huyo aliye nipiga risasi zote hizo atafutwe na ashughulikiwe kisheria,”amesema.

Kuhusu kuingia na kutoa nchini mara kwa mara ameeleza kuwa ni kawaida yake na kwamba swala hilo lisichukiliwe kama ni hofu ya usalama wake.

“Nafanya kazi za kimataifa ,safari zangu zipo Vilevile kama ilivyokuwa mwanzo,jumamosi iloyopita nilitoka Ulaya na mwezi ujao nitaenda mara mbili Ulaya ni kawaida isichukuliwe kitofauti”amesema Mwanasiasa huyo.

Gari ambalo Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi akiwa ndani yake Septemba 7, 2017

Katika hatua nyingine Makamu Mwenyekiti huyo amezungumzia kukwama kwa mchakato wa Katiba Mpya kuwa kinachoendelea ni maneno tu na hakuna vitendo.

Amesema ili wao wamwamini Rais aliyepo madarakani ni wanahitaji kuona matendo zaidi kuliko maneno.

Kuhusu mahali aliko dereva ambaye alikuwa naye wakati anashambuliwa Lissu amesema yuko nchini Uberigiji na kwamba alipelekwa huko kutokana na sababu za usalama wake kuwa kwenye mashaka .

“Dereva wangu Nilienda naye Uberigiji,amesimeshwa huko na kujua lugha mpaka ananishinda mimi,maneno ya kusema amekimbia nchi yake ni ya kijinga muda wowote akitaka atarudi hapa ni kwao,”amesema

Please follow and like us:
Pin Share