Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango na mkewe mama Mbonimpaye Mpango wameungana na waumini wengine katika kushiriki Ibada ya kawaida ya asubuhi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Fransisco Nzavery -Nyakahoja Jijini Mwanza. Ibada iliyoongozwa na Padre Victor Awiti.

Akiwasalimu waumini mara baada ya ibada hiyo leo Aprili 12,2023, Makamu wa Rais amewasihi wakristo na watanzania kwa ujumla kujitafakari tena katika namna ya kukabiliana na mmomonyoko wa maadili.

Amesema mfumo mzima wa maadili kuharibika umepelekea ubadhirifu wa fedha za umma hivyo ni vema kuendelea kulinda maadili mema ya kitanzania kwa kuwapa miongozo watoto na kufuatilia mienendo yao wakati wote.

Aidha Makamu wa Rais ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa pamoja na viongozi wa serikali ili waweze kuongoza vema taifa kwa hekima ya Mungu.

Makamu wa Rais yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo mkoani humo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasalimu waumini waliohudhuria Ibada ya kawaida ya asubuhi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Fransisco Nzavery -Nyakahoja Jijini Mwanza leo tarehe 12 Aprili 2023
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Ibada ya kawaida ya asubuhi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Fransisco Nzavery -Nyakahoja Jijini Mwanza leo tarehe 12 Aprili 2023.
Please follow and like us:
Pin Share