Serikali ya Uingereza imeongeza kiwango cha tahadhari kuhusu kitisho cha kutokea mashambulizi ya kigaidi katika jimbo la Ireland ya Kaskazini kabla ya ziara inayotarajiwa ya Rais Joe Biden wa Marekani.
Rais huyo wa Marekani anatarajiwa kuhudhuria kumbukumbu ya miaka 25 tangu yalipofikiwa makubaliano ya amani ya kihistoria, Aprili 10 mwaka 1998 yanayotambuliwa kama “Makubaliano ya Ijumaa Kuu”, ambayo yalimaliza machafuko ya umwagaji damu Ireland Kaskazini.
Kwa mujibu wa kiongozi mkuu wa Ireland Kaskazini, Chris Heaton-Harris, Shirika la Ujasusi la Uingereza (MI5), linaamini kitisho cha kutokea mashambulizi ni kikubwa.
Ametoa mwito kwa umma wa Ireland Kaskazini kuwa makini lakini pia kutotaharuki kufuatia tangazo hilo.