Askari wa kutuliza ghasia nchini Kenya wako katika mitaa ya mji mkuu, Nairobi, katika jitihada za kuzuia maandamano yaliyoitishwa na upinzani kuhusu gharama ya juu ya maisha na madai ya ukiukwaji wa maadili katika uchaguzi.

Pia kuna idadi kubwa ya polisi katika Kibera na Mathare – makazi ya mabanda yasiyo rasmi na makubwa zaidi katika jiji – ambapo waandamanaji wanazuiwa kuinga katikati mwa jiji.

Gari lililokuwa limebeba wanahabari wa eneo la Kibera lilishambuliwa na umati wa watu na waliokuwa ndani yake kuibiwa kwa kuchomwa visu na kujeruhiwa, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini.

Maduka yamefungwa katikati mwa jiji la Nairobi huku wamiliki wa biashara wakihofia uporaji.

Katika mji wa magharibi wa Kisumu, ngome ya upinzani, vitoa machozi vimerushwa kutawanya umati wa waandamanaji waliokuwa wakiongozwa na gavana wao wa eneo hilo.

Polisi wamesema watawapiga picha waandamanaji na kuwafungulia mashtaka kwa kushiriki maandamano haramu