Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Stephen Wassira kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), kwa kipindi cha pili cha miaka minne baada ya kipindi cha kwanza kumalizika; na
Amemteua Dkt. Fidelice Mbaruku Simbagungile Mafumiko, kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano (05) kuanzia tarehe 03 Aprili, 2023.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu