Malawi ndio nchi iliyoathirika zaidi na kimbuga hicho, ambapo watu hadi sasa 99 wamepoteza maisha yao kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosomba nyumba kadhaa nchini humo.
Kamishna katika Idara ya Kukabiliana na Majanga Charles Kalemba amewaambia waandishi wa habari kuwa, wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.
Kalemba ameeleza kuwa, watu 134 wamejeruhiwa na wengine 16 hawajulikani waliko. Tayari mji mkuu wa kibiashara wa Malawi Blantyre umerekodi vifo 85 viliyotokana na kimbunga hicho.
Shughuli za uokozi zingali zinaendelea huku wakaazi wakiripotiwa kutumia mikono yao kuchimba wakiwa na matarajio ya kupata manusura zaidi.