Takribani watu 7 nchini Madagascar na 7 nchini Msumbiji wamepoteza maisha baada ya kimbunga Freddy kupiga.
Kulingana na ripoti ya hivi punde ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), idadi ya watu walioathiriwa na Kimbunga Freddy imeongezeka hadi 383, 000 (226,000 nchini Madagascar na zaidi ya 163,300 nchini Msumbiji).
“Ijapokuwa nguvu ya Kimbunga Freddy haikuwa kama tulivyotarajia, mamia ya maelfu ya watu wanahitaji msaada wa kibinadamu . Ahueni itachukua miezi kadhaa, “Pasqualina Di Sirio, Mwakilishi wa WFP na Mkurugenzi wa Nchi wa Madagascar aliiambia BBC.
Kuna uwezekano wa mafuriko kusini-mashariki mwa Zimbabwe kwani kimbunga Freddy hakikuweza kuenea kama ilivyotabiriwa awali.