Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi kwa kuwateua Wawaziri na Naibu Waziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kuwahamisha wizara baadhi ya Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu pamoja na kumteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Aidha Rais amefanya uhamisho wa Mkuu wa Mkoa mmoja.Katika mabadiliko hayo,Rais amefanya uhamisho wa mkuu wa mkoa mmoja. Katika mabadiliko hayo rais amehamishia majukumu ya Uwekezaji katika Ofisi ya Rais .Vilevile amefuta nafasi ya Katibu Mkuu (Uvuvi) na badala yake Wizara ya Mifugo na Uvuvi itakuwa na Katibu Mkuu mmoja (Uvuvi),na wizara hiyo itakuwa na Katibu Mkuu mmoja na Naibu Makatibu Wakuu wawili.

Kati ya viongozi wapya walioteuliwa ni Mbunge wa Muheza ambaye pia ni msanii wa Hip Hop,Hamis Mohamed Mwinjuma ‘Mwana FA’ kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumapili Februari 26, 2023 na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa Mwana FA amechukua nafasi ya Pauline Gekul ambaye amehamishwa kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.

Mwana FA aliingia kwenye siasa na katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020 akafanikiwa kushinda nafasi ya ubunge wa Muheza, Tanga.

Pia amemteua Christina Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo anachukua nafasi ya Sophia Mjema ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi-Itikdi na Uenezi

KWA TAARIFA ZAIDI SOMA HAPA https://www.jamhurimedia.co.tz/rais-samia-afanya-mabadiliko-baraza-la-mawaziriwakuu-wa-mikoa-atengua-na-kuteua-wengine/