Na Mwamvua Mwinyi,JamhuriMedia,Mapinga

Mwenyekiti wa kamati ya Usalama mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge, amesema Serikali inaendelea kusimamia Maamuzi ya hukumu za mahakama katika migogoro ya ardhi kata ya Mapinga ,na hawawezi kuipinga mahakama .

Amewashauri walioshinda mashauri yao kuona kama inafaa waketi meza moja ili kufanya maridhiano .

Akitoa msimamo wa Serikali na kamati iliyoundwa na Waziri wa Ardhi Angelina Mabula,kushughulikia migogoro iliyokithiri kata Mapinga ,Kunenge akiwa kwenye utekelezaji eneo la Kiharaka, aliwaasa wananchi 250 wanaodaiwa kuingilia eneo halali la Balozi Saimon Mlai wanaondoke kama maamuzi ya Mahakama Kuu yalivyoamua.

“Wale ambao mmeshinda kesi na tayari mahakama zimetoa tuzo na kuteua dalali kwa kutekeleza ni kazi ya Serikali kusimamia hukumu ya Mahakama na sio kuingilia au kusikiliza kesi upya.

“Sisi hatulazimishi mzungumze kukubaliana ,ni Maamuzi ya aliyeshinda kesi kuona Kama inafaa kuzungumza na wananchi, na Kama yupo ambae hajaridhika na maamuzi ya mahakama wakakate rufaa “

Kunenge,alieleza Mahakama ilituma dalali kuja kuwaondoa wananchi wavamizi,na eneo ni mali halali ya Balozi Mlai,mwenye hati halali ambayo haijabatilishwa.

Mwakilishi wa wananchi Jeremiah Mtema alisema, wapo tayari kwa maridhiano na wenye eneo ili maisha yaendelee.

Kufuatia kauli hii, Kunenge ametoa wiki wananchi kuonana na mwenye mali kuangalia namna ya kumaliza tatizo Hilo Lakini ambae hataki maridhiano aondoke kupisha eneo.

Vilevile Kunenge alifika eneo lenye mgogoro baina ya Taasisi ya Kijiko na wananchi 15 wanaodaiwa kuvamia eneo hilo, ambapo aliwataka wananchi waache kuendeleza chochote Cha maendeleo na Kwa upande wa Kijiko wasiwabughudhi wananchi hadi hapo Suluhu la mahakama au maridhiano litakapokamilika.

“Katika mgogoro huu, hakuna mwenye haki hadi sasa,hivyo ushauri ni kwenda kufungua kesi ili haki itendeke” amesema.

Pili aidha wanaweza kukaa meza moja ili kuweka maridhiano ,na upande wa Serikali kutakuwa na watalaam ambao watasimamia, hatimae mgogoro huu uishe na kila mmoja aendelee na maendeleo yake.

Akiwa eneo la Mtambani,Kunenge ameeleza ,Tume iliyoundwa na Waziri wa Ardhi Angelina Mabula ilipokea malalamiko ya baadhi ya walalamikaji ambao mashauri yao yaliisha mahakamani na dalali kuteuliwa ,na hakuna mpingaji ,maoni ya kamati kwenye Maamuzi ambayo mahakama imeshafanya maamuzi na kuteuliwa dalali na kuanza kazi yake wananchi hao wanatakiwa waondoke.

Kunenge ameeleza,wapo wengine kesi zimeisha na wanapaswa kuzikazia hukumu zao ili haki itendeke na mashauri yanayoendelea mahakamani, kusubiri Maamuzi .

Please follow and like us:
Pin Share