Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeibuka mshindi wa kwanza kwa Taasisi zenye uhusiano mzuri na vyombo vya habari, TRA imeshika number mbili na CRDB imekuwa ya tatu, Tuzo hiyo imetolewa na Chama cha Maafisa Uhusiano Tanzania, Dar es Salaam.

Sambamba na hilo pia Meneja wa Mawasiliano EWURA, Titus Kaguo, ameibuka kuwa mtendaji bora wa Mawasiliano na Uhusiano katika sekta ya mafuta na gesi Tanzania.

Tuzo hizo zimefunguliwa na na Naibu Waziri wa Habari, Kundo Mathew na kuhudhuriwa na Wataalamu wa Habari na Mawasiliano wa Serikali na sekta binafsi

Please follow and like us:
Pin Share