Na Mwanadishi Wetu,JamhuriMedia

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI kwa kushirikiana na Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo zimeendesha kliniki maalum (MOI Mobile clinic kwa wa kazi wa Bagamoyo ambapo zaidi ya wagonjwa 150 wamehudumiwa.

Kliniki hiyo imehusisha huduma za kibingwa na kibobezi za mifupa , Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu.

MOI ina ilianzisha Kliniki ili kutekeleza agizo la Serikali ya awamu ya Sita kupitia Wizara ya Afya la kuhakikisha huduma za kibingwa zinasogezwa karibu na wananchi.

Daktari bingwa wa Mifupa MOI Dkt.Bryson Mcharo amesema mwitikio wa wakazi wa Bagamoyo ni mkubwa hivyo anawasihi wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kupata Matibabu katika kliniki hiyo watakaposikia matangazo.

Dkt. Mcharo amesema asilimia kubwa ya wagonjwa waliojitokeza ni wananchi wenye changamoto za mifupa na maumivu ya Mgongo pamojq na mishipa ya fahamu na magonjwa mengine.

“Tumewasogezea wananchi huduma katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kwani tunatoa huduma kwa wakazi wa Pwani kupitia kliniki yetu pendwa ‘MOI Mobile Clinic’ kwani wananchi wanahitaji sana huduma za kibingwa na kibobezi Alisema Dkt Mcharo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo Dkt Luiyana Lymo ameushukuru uongozi wa MOI kwa kushirikiana na hospitali yake kuwahudumia wananchi na kuwapunguzia usumbufu wa kufuata huduma hizo MOI.

Mkazi wa Bagamoyo Mwanaidi Athumani ameishukuru Taasisi ya MOI kwa kusogeza huduma karibu na hivyo Taasisi nyingine za afya ziige mfano wa MOI kwani sio watanzania wote wanaoweza kufuata huduma hizo MOI.

Please follow and like us:
Pin Share