Viongozi wa vyama vya siasa nchini wameaswa kushirikiana ili waweze kujenga mazingira mazuri ya kufanya siasa zenye tija na siasa za kushindana kwa hoja.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Ibrahim Lipumba leo Februari 06, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua Jukwaa la Majadiliano Wilaya ya Ilala kwa lengo la kuwaunganisha viongozi wa vyama vya siasa katika wilaya hiyo kwa ajili ya kuanza majadiliano ya pamoja katika kuunda mshikamano na umoja.

Amesema jukwaa hilo litawezesha majadiliano na jinsi ya kuendeleza demokrasia,amani na kuendeleza maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Majadiliano Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari06, 2023.

“Kitaifa tuna jukwaa la vyama, tunakutana na viongozi wa vyama vya siasa kwa ngazi ya wilaya ili kuendeleza Demokrasia na kuweza kubadilishana mawazo ni namna gani ya kuendeleza Demokrasia na kuweza kujadiliana namna ambavyo shughuli zetu za kisiasa tunazifanya kwa mujibu wa taratibu na sharia na kwaamani,” ameeleza Prof.Lipumba.

Katika jukwaa hilo wamesisistiza kwamba mambo ya msingi hasa kuwepo ni kuwa na tume huru ya uchaguzi, nimhimu ili tuweze kuwa na amani endelevu.

“Kama nchi na taifa tunahitaji kujadiliana ili tuweze kuapata tume huru ya uchaguzi ambayo itakuwa na uwezo wa kusimamia chaguzi za serikali za mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025,” ameeleza Prof. Lipumba.

Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Manachama wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 06, 2023 jijini Dar es Salaam. mara baada ya kuzindua JukwaaMajadiliano Wilaya ya Ilala.

Amesema hayo ndio mambo ya kitaifa na jukumu la Serikali katika hatua ya wilaya, tunahitaji viongozi wetu wa vyama waweze kushirikiana kujenga mazingira mazuri ya kufanya siasa zenye tija, siasa za kushindana kwa hoja.

Pia Prof.Lipumba amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuwa na maridhiano ya majadiliano na vyama vya siasa nchini ikiwa ni pamoja na kuruhusu vyama vya siasa nchini vifanye kazi zake kwa uhuru na amani.

Amesema Rais Dkt.amia ameruhusu mambo manne katika utekelezaji wa kazi za vyama vya siasa katika vipengele vine ambavyo ni Maridhiano,ustahimilivu,mabadiliko na ujenzi mpya wa Taifa.

Kwa Upande wa Msaidizi wa Masuala ya Siasa na Uchumi, Ubalozi wa Marekani,Bion Bliss amesema kuwa Marekani inashirikiana na washirika wake katika kuhakikisha demokrasi inaimarika, wanachi wanakauli na kuweza kuchagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi huru,amani, haki na uaminifu.

Mkurugenzi wa TCD, Bernadetha Kafuko, Akitoa ufafanuzi juu ya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) jijini Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa Jukwaa la Majadiliano Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari06, 2023.

Amesema jukuwaa hili litawanguanisha viongozi wa vyama vya siasa ili kuweza kuafanya siasa,Kuwa na vipaumbele vya pamoja ikiwemwo mazungumzo ya pamoja ili kuleta uelewa wa pamoja kwa wananchini wake.

Akizungumzia kuhusiana na majadiliano ya pamoja na viongozi wa vyama vya siasa, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa jukwa hilo litakuwa eneo muhimu la kuwaweka pamoja viongozi wa vyama vya siasa ili kujadiliana changamoto mbalimbali na kuweza kupata majawabu wakiwa mezani.

“Naamini kwamba Chini ya Uongozi wa TCD chini ya Mwenyekiti wake, Abraham Kinana na Makamu Mwenyekiti, Prof. Lipumba nchi hii itakaa kwenye meza ya majadiliano ya pamoja, tuwaombee kuelekea kwenye maridhiano na majadiliano.” amesema Zitto.

Msaidizi wa Masuala ya Siasa na Uchumi, Ubalozi wa Marekani, Bion Bliss akizungumza wakati wa wa Uzinduzi wa Jukwaa la Majadiliano Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari06, 2023.