Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

(1) Amemteua Bi Janet Zebedayo Mbene kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

(2) Amemteua Bw. James Andilile Mwainyekule kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Bw. Mwainyekule ni Mhasibu Mkuu, Tume ya Pamoja ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango, Dodoma.

(3) Amemteua Bw. Rashid Kassim Mchatta kuwa Skauti Mkuu Tanzania. Bw. Mchatta anachukua nafasi ya Bi. Mwantumu Mahiza ambaye muda wa kutumikia nafasi hiyo umemalizika.

(4) Amemteua Bw. Gilead John Teri kuwa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Bw. Teri ni Mshauri Mwandamizi, Umoja wa Ulaya (EU), Copenhagen, Denmark.

(5) Amemteua Bw. Damasi Joseph Mfugale kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Bw Mfugale ni Mshauri Mwandamizi wa Kampuni ya Afrika Chapter EBI International Consulting Group, Canada.

(6) Amewateua Makamishna wa Tume wawili (2) kama ifuatavyo:-

(i) Bi. Caroline Joseph Mutahanamilwa kuwa Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania; na

(ii) Bw. Idd Ramadhan Mandi kuwa Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Februari, 2023.

Zuhura Yunus

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu