Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya Wapya 37, kuwahamisha vituo vya Kazi Wakuu wa Wilaya 48 na wengine 55 kubakia kwenye vituo vyao.
Kati ya Wakuu wa Wilaya hao 140, Wanawake ni 40 na Wanaume ni 100 ambapo miongoni mwa wakuu wa Wilaya wapya walioteliwa ni pamoja na;

Rais Samia amewateua; aliyekuwa Katibu wa Halimashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (NEC) Shaka Hamdu Shaka kuwa mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Victoria Charles Mwanziva kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Jaffar Haniu Mkuu wa Wilaya Rungwe, na Grace Kingalame kuwa Mkuu wa Wilaya Nyang’wale.

Baadhi ya Wakuu wa Wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya Temeke Jokate Urban Mwegelo, amepelekwa Wilaya ya Korogwe, Nick Simon (Nikki wa Pili) Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amehamishiwa Kibaha, Fatma Almas Nyangasa, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni amehaimishiwa Kisarawe naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Crydon Gondwe amehamishiwa Wilaya ya Bahi.