Binadamu mzee zaidi aliyekuwa anashikilia rekodi ya Guinness amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 118.
Sista André aliyezaliwa Februari 11, 1904 na kupewa jina la Lucile Randon amekutwa amefariki katika makazi yake yaliyoko mjini Taulon Ufaransa, Reuters imeripoti
Msemaji wa makazi ya watawa ya Sainte Catherine Labourre Nursing Home David Tavella amesema Mtawa huyo amefariki akiwa usingizini
“Kuna huzuni kubwa lakini ilikuwa ni haja ya moyo wake kuungana na Kaka yake kipenzi”amesema Tavella
Sister André alitajwa katika rekodi ya dunia ya Guinness kuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani mwezi April 2022 baada ya kifo cha Tanaka raia ya wa Japan aliyekuwa na umri wa miaka 119.
Pia ndiye mtawa aliyeishi kwa mda mrefu zaidi na Mfaransa wa pili kufariki katika umri huo
Kabla ya kuwa mtawa, alitumika kuwahudumia watoto yatima katika kipindi cha vita ya pili ya dunia na mara baada ya vita aliendelea kuwatunza wazee na watoto yatima hospitalini.