Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Tanzania imejipanga kuchukua hatua katika kuhakikisha uchumi wake unaendelea kukukua pamoja na kusimamia urekebishwaji wa baadhi ya sera.
Hayo katika mafunzo maalumu kwa wahariri wa vyombo mbalimbali kuhusiana na mwenendo wa uchumi wa dunia na namna Tanzania inavyoathiwa yaliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaliyofanyika leo Januari 16,2023 mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza katika mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Lawrence Mafuru,amesema kuwa unapozungumzia uchumi wa dunia ni lazima utaizungumzia nchi China kwa kuwa ni nchi ambayo uchumi wake ni mkubwa.
“Unapozungumzia uchumi wa dunia huwezi kukwepa kuizungumzia China kwani ni nchini yenye uchumi mkubwa duniani lakini pia zipo nchi ambazo nazo ni lazima uzizungumzie unaelezea masuala ya uchumi duniani,” amesema Mafuru.
Amesema kuwa China inaposhuka uchumi wake kuna nchi ambazo huathirika na kusababisha changamoto mbalimbali kama kuibuka kwa mfumuko wa bei, kupanda kwa riba katika benki, changamoto ya ajira, kuwepo kwa vikwazo vya dunia.
Amesema kuwepo kwa vita kati nchi ya Ukraine na Urusi pia kumeathiri pia katika kushuka kwa uchumi wa dunia lakini pia suala la ugonjwa wa COVID nalo limethiri nchi nyingi duniani uchumi wake kushuka.
“Katika kipindi hiki cha COVID nchi nyingi uzalishaji wake ulishuka hivyo kumesababisha uchumi wa nchi nyingi kushuka kwani wananchi walikuwa lockdown, bidhaa kutosafirishwa na kutofanyika kwa biashara mbalimbali,” amesema.
Mafuru amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa Tanzania uchumi wake unasonga mbele ni wakati sasa wa wananchi kupata kufahamu fursa zilizopo nchini na ambazo zitachochea uchumi wa nchi kusonga mbele.
Ameongeza kuwa ili kuboresha uchumi watapitia sera,kodi na nyanja mbalimbali ambazo zinaathiriri sekta ya uchumi ili kusukuma mbele uchumi wa Tanzania hivyo zinapaswa kuungwa mkono ili kukuza ukuaji wa uchumi wa ndani katika nyakati hizi za msukosuko.
Naye Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Suleiman Missango kutoka BoT amesema kuwaukuaji wa uchumi zinatokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa jumla katika taifa ambapo mapato yake yanatofautiana katika kumwendea kila mmoja kutegemeana na shughuli za uzalishaji.
Amesema kuwa takwimu za ukuaji wa uchumi zinatokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa jumla katika taifa hivyo katika kuhakikisha Tanzania uchumi wake unasonga mbele ikiwa ni pamoja na kupata mikopo ipo haya ya wananchi kushiriki kikamilifu kwa kufahamu fursa zitakazosaidia kusongesha maendeleo.
“Katika sekta ya utalii tayari rais Samia Suluhu Hassan ameingia katika mapambano kwa kushiriki kwenye filamu ya Royal Tour kwani imesaidia kuongeza idadi ya watalii lakini pia ni wakati sasa kwa wananchi kushiriki katika suala la zima na utunzaji mazingira kwani ni kati ya vigezo ambazo nchi inapata mikopo kutokana na makubaliano yaliyofikiwa hata hivyo Tanzania tupo katika nchi inayokopesheka,” amesema Missango.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodutus Balile ameishukuru Benki Kuu (BoT), kuandaa mafunzo hayo ambayo yatasaidia wahariri katika utendajikazi wao.
“Haya mafunzo ni vyema yakawa endelevu kwani yatasaidia sana wahariri katika kufanyakazi kwa umahiri hivyo ni kuwepo kwa mafunzo haya ni njia mojawapo ya kusaidia jamii kupata elimu kuhusiana na masuala ya uchumi kupitia vyombo vya habari,” amesema Balile.