Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema, uhuru wa vyombo vya Habari hukuza demokrasia Nchini
Ametoa kauli hiyo akizungumza na baadhi ya waandishi leo Januari 16,2023, jijini Dar es Salaam.
Amesema kukiwa na demokrasia basi vyombo vya habari vitakuwa huru kwa sababu sheria zitakua nzuri sio za ukandamizaji hivyo watu watakua huru kutoa mawazo na kukosoa.
Pia ametaja mambo mbalimbali ambayo yatasaidia nchi ikiwa vyombo vya habari nchini vitakuwa huru.
Amesema Serikali ina nafasi nzuri ya kuweza kujitathmini katika utendaji wao ja kuangalia kama wanakwenda vizuri au hawaendi sawa sawa.
“Vyombo vya habari ni kama kioo kwa serikali na sekta binafsi, hivyo vikiwa huru vitaweza kusaidia serikali kufanya tathmini ya utendaji kazi wake” – Sheikh Ponda