Ikiwa ni siku chache tu baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jatu PLC kufikishwa mahakamani kutokana na
tuhuma zinazomkabili za matumizi mabaya ya ofisi, uongozi wa kampuni hiyo kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi
Mohamed Simbano, wamemtambulisha mtaalamu wa masuala ya fedha na uwekezaji kutoka Uholanzi Ben Philipsen kwa ajili ya kutengeneza mpango mkakati wa kuinusuru kampuni hiyo pamoja na mitaji iliyowekezwa na wawekezaji na wanahisa katika kampuni hiyo.
Mtalamu huyo ametokea kwenye taasisi ya PUM Netherland Expet ambao ni wazoefu katika nyanja ya masoko , mitaji na
uwekezaji nchini Uholanzi hivyo wakiwa hapa watashrikiana na wadau na washirika mbalimbali wanaofanya kazi na Jatu ili waone ni namna gani wataweza kukuza mitaji na kumaliza madeni.
Imeelezwa kuwa, mtaalamu huyo pia atatoa ushauri wa namna ya kuendesha miradi iliyokuwepo awali na kuisimamia kwa weledi na kwa ujuzi utakaoleta tija na kumaliza changamoto zilizokuwepo, pia kampuni hiyo itashirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi ambao ni wanahisa, wakulima, washauri, taasisi za Serikali na wahisani ili kukamilisha mchakato wa kuleta mabadiliko katika kampuni.

Mshauri huyo mwelekezi, Ben Philipsen amesema amekuja nchini kwa ajili ya kuangalia namna gani atatumia uzoefu wake katika kuandaa mikakati itakayoinua ameongeza kwa kusema Jatu inaingia kwenye mkakati mpya na wenye maoni mkubwa hasa ukizingatia kuwa kampuni hiyo imeorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE).

Aidha katika kuhakikisha shughuli za Jatu Plc zinarudi na kuendelea kama ilivokuwa hapo awali kumekuwa na vikao vya mara kwa mara baina ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Jatu kwa miezi mitatu mfululizo kati ya Septemba hadi Novemba hali iiyopelekea mpaka sasa ofisi za Jatu zote zilizokuwa hazifanyi kazi kufunguliwa na kuanza kufanya kazi ikiwemo ofisi ndogo ya Vingunguti ambayo kwa sasa imerejesha shughuli zake za uzalishaji wa unga wa dona pamoja na ofisi za makao makuu kurudi katika eingo la PSSSF ghorofa ya 11.
Vilevile Mwenyekiti wa Bodi ya JATU, Dk Zaipuna Yohana nae amesema hakuna hela iliyowekezwa katika kampuni hiyo
itakayopotea kwani mpango mkakati wao kwa mwaka huu ni kuongeza juhudi katika kilimo ili kuongeza mapato na
kupunguza madeni.