Hivi karibuni kumekua na taarifa za uzushi na upotoshaji zinaendelea kutolewa kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya

watu wenye nia ovu ili kuzua taharuki kuwa ndege zinazoruka na kutua katika maeneo ya hifadhi zinasafirisha wanyamapori na rasilimali nyingine zinazolindwa na kuhifadhiwa kisheria.

Taarifa hizo sio za kweli tunaomba wananchi mziipuze. Kama tunavyofahamu Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kwa kuwa na

vivutio vingi vya utalii zikiwemo Hifadhi za Taifa 22, Mapori ya Akiba 22, Mapori Tengefu 29, Hifadhi ya Ngorongoro,

Hifadhi za Misitu, maeneo ya kihistoria na urithi wa dunia, Hifadhi za Bahari na fukwe, maziwa makuu, mito na maeneo

mengine mengi ya asili. Maeneo haya ya vivutio yamekuwa yakitembelewa na watalii wa aina mbalimbali na kuliingizia Taifa fedha za kigeni pamoja na kuzalisha fursa za ajira.

Aidha, watalii wengi wamekua wakiitembelea Tanzania kutokana na juhudi kubwa za kutangaza utalii zilizofanyika ambazo

zimekua kichocheo cha shughuli mbalimbali zikiwemo za utalii wa picha, safari za parachuti (balloon), kutembea nyikani,

kupanda milima, utalii wa fukwe na utalii wa utamaduni.

Kutokana na umuhimu wa shughuli hizo, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya maboresho makubwa ya

kufungua na kukarabati miundombinu ya Utalii vikiwemo viwanja vya ndege, barabara na miundombinu mingine muhimu

katika maeneo ya hifadhi ili kuwezesha uendelevu wa shughuli za uhifadhi pamoja na kuiwezesha Sekta Binafsi kutoa

huduma ya usafiri wa ndege zinatua na kuruka kwa nyakati tofauti zikiwa zimebeba watalii kutoka katika viwanja vikubwa

hususani Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam (JNIA), Kilimanjaro (KIA) na Abeid Amani Karume

International Airport , Zanzibar.

Kwa muktadha huu, Wizara ya Maliasili na Utalii inawahakikishia Watanzania kuwa viwanja vyote vya ndege vilivyoko

katika maeneo ya hifadhi viko salama na vinatumika kwa shughuli za usafirishaji wa watalii wanaotoka katika maeneo

mbalimbali hapa nchini.

Aidha, Wizara iko makini kuhakikisha matumizi sahihi ya viwanja hivyo kwa wageni wote wanaoingia na kutoka katika

maeneo ya hifadhi.

Tunawaomba wananchi muwe watulivu na kuwa makini na watu wanaotoa taarifa za upotoshaji na za kichochezi zisizo

rasmi kuhusu ndege na matumizi ya viwanja hivyo.

Aidha, tunawaomba wananchi mnapoona matumizi yasio sahihi msisite kutoa taarifa kwenye vituo vyetu vya uhifadhi, vituo vya Polisi au ofisi za Serikali zilizo katika maeneo yenu ili kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali zetu.