Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne na kidato cha pili uliofanyika Oktoba na Novemba mwaka jana.
Akisoma Matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari , leo Januari 4, 2023 jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Amasi amesema jumla ya wanafunzi 1,718, 896 walisajiliwa kufanya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne, wasichana 807,999 sawa na asilimia 50.67 na wavulana 8,478,97 sawa na asilimia 49.33.
Na kwa upande wa kidato cha pili jumla ya wanafunzi 609,341 walisajiliwa kufanya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili wakiwemo wasichana 367,013 sawa na asilimia 53.16 na wavulana 323,328 sawa na asilimia 46.84.
“Darasa la nne jumla ya wanafunzi 1,718, 896 walisajiliwa kufanya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne wsichana 807,999 sawa na asilimia 50.67 na wavulana 847,897 sawa na asilimia 49.33” amesema Athumani.
“Kwa upande wa upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili jumla ya wanafunzi 60,9341 walisajiliwa kufanya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili wakiwamo wasichana 3,68,013 sawa na asilimia 53.16 na wavulana 323,328 sawa na asilimia 46.84.”amesema.
Kaimu Katibu Mtendaji huyo amesema kati ya wanafunzi waliosajiliwa, wanafunzi 635,130 sawa na asilimia 92 walifanya upimaji huo na jumla ya wanafunzi 1,262,96 sawa na asilimia 7.33 hawakufanya upimaji
“Kati ya wanafunzi waliosajiriwa, wanafunzi 1,592,600 sawa na asilimia 92.65 walifanya upimaji huo wakiwemo wasichana 819,675 sawa na asilimia 94.11 ya wasichana waliosajiriwa na wavulana 772,925 sawa na asilimia 91.16 ya wavulana waliosajiriwa.”amesema
“Jumla ya wanafunzi 1,262,96 sawa na asilimia 7.33 hawakufanya upimaji na kati yao wasichana ni 513,224 sawa na asilimia 5.89 na wavulana ni 74,972 sawa na asilimia 8.84.”amesema
Aidha amesema kwa upande wa kidato cha pili kati ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya upimaji wa huo ni wanafunzi 6,350,130 sawa na asilimia 92 walifanya upimaji huo, ambapo jumala ya wanafunzi 55,211 saa asilimia 8 hawakufanya upimaji.
“Kati ya wanafunzi waliosajiriwa kufanya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili wanafunzi 6,350,130 sawa na asilimia 92 walifanya upimaji huo, wakiwemo wasichana 342,210 sawa na asilimia 92.24 ya wasichana walossajiriwa na wavulana 929,20 sawa asilimia 90.6 ya wavulana waliosajiriwa.” amesema
“Jumala ya wanafunzi 55211 saa asilimia 8 hawakufanya upimaji na kati yao wasichana ni 24803 sawa na asilimia 6.76 na wavulana ni 30408 sawa na asilimia 9.40.”amesema
Pia Kaimu Katibu Mtendaji huyo amesema, wanafunzi 442 wa darasa la nne na 258 wa kidato cha pili yamezuiliwa kutokana na wanafunzi hao kushindwa kukamilisha mitihani yao kwa sababu za matatizo ya kiafya.