Na Aziza Nangwa,JamhuriMedia

Nchi 15 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika zipo nchini, kushiriki kongamano la kutoa uelewa mpana juu ya mkataba wa kimataifa kwenye suala zima la kulinda mazingira ya bahari yaweze kuwa endelevu kwa viumbe wa majini.

Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo mkurugenzi mkuu Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC ),Kaimu Mkeyenge amesema lengo kutano huo ni wadau kupata uelewa juu mkataba wa kimataifa, ambapo nchi wanachama wanatakiwa kufuata na kuweka sheria na kanuni katika nchi zao jinsi ya kuzibiti maji ambayo huwa yanatumika katika vyombo vya usafiri wa majini kwa maana ya meli ili ziweze kupata balance yasiweze kuathiri viumbe walipo baharini.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya uchukuzi) Dkt. Ally Possi akizungumza na waandishi wa habari mara baada kufungua warsha ya Siku tatu kwa wadau wa Bahari jana jijini Dar es Salaam

“Haya maji huwa yanawekwa katika vyombo kama meli ili inapofika,kwenye bandari ambayo inahisi maji yale yanatakiwa yatolewe kuwe na balance ya mizigo ambao utabebwa yanatakiwa yashushwe,” anasema Mkenyenge.

Amesema maji yale yakikaa sana,kuna uwezekano wa kuzalishwa viumbe ambavyo zitakuwa hatarishi,pindi yanaposhushwa baharini na katika eneo ambalo ni maji ya kitaifa au sehemu yayote majini .

Hivyo basi viumbe hivi hatarishi visipo thibitiwa vilivyopo baharini vitakuwa hatarini na sisi tuna vihitaji kwa maendeleo ya uchumi wa bluu, unaweza usifikiwe kwa maana kama mazingira ya maji hayadhibitiwi kwenye suala zima la utunzaji.

Pia kunaweza kusababisha kututofikia uchumi wa bluu kama mikataba hii, hatutoiridhia na kuzingatia ni jinsi gani ya kujikinga na viumbe hivyo ambavyo vitazalishwa na maji haya
Wito ni kutoa uelewa kwa taasisi mbalimbali, zinazohusika na maswala ya bahari na maji wawe na uelewa wa pamoja ili pale ambapo tutakapofika na kuridhia mkataba huu na kutengeneza kanuni za kutumika hapa nchini somo liwe tayari limefahamika vizuri.

Naibu katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi Dkt Ally Possi amesema Tanzania kama mwanachama umoja wa kimataifa, ina wajibu wa kuhakikisha mazingira ya majini au vyombo vinavyofanya safari kama meli havichafui bahari.

Dkt.Possi amesema mkutano una umuhimu wa kuzingatia makubalino ya itifaki ambayo ilipitishwa mwaka 2014 na kuanza kutumika 2017 na Tanzania ni moja ya mwanachama wa umoja huo wa kimataifa, kwa hiyo tunawajibu sasa kuhakikisha mazingira na vyombo vyetu vya majini havichafui bahari ,maziwa na mito.

“Hali kwa sasa ni nzuri lakini lazima kuchukua tahadhali kwa ajili ya maendeleo ya vizazi vijavyo ndiyo maana wito wa wanachama ni mkubwa na kwasasa,ndilo jambo ambalo dunia imeanza kulipa kipaumbele katika kuhakikisha mazingira katika maji hasa bahali,mito na maziwa yetu yanatunzwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

lakini pia vyanzo vya maji hususani bahari vinasimamia uchumi wa bluu sasa bahari inapochafuka inapohalibiwa sera ya uchumi wabluu inakuwa ngumu kutekelezeka ,kwasababu viumbe ambavyo vitafanyiwa uchumi wa bluu kama samaki vitatoweka na mazingira yataharibika na kushindwa kufanya kazi inayotakiwa.

Baada ya mkutano huu tutarajie sio tu Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla, kutakuwa na uelewa mpana kwa wadau wote waliopo hapa mwishowe watapeleka ujumbe.

Amesema wataalamu wanatuambia uchafuzi wa mazingira majini una athari , unategemea kuzalisha viumbe ambavyo vitakuwa hatarishi kwa viumbe vitakavyokuwa baharini.

Mkurugenzi wa Usalama na mazingira baharini kutoka Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stela Katondo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

Kongamano hilo limeandaliwa na Shirikala la Bahari la Kimataifa International Marinetime Organization (IMO )na kuratibiwa na Wakala wa meli Tanzania (TASAC ) kama mwenyeji wa kongamano hilo.