Timu ya Taifa ya Morocco imeandika historia katika Bara la Afrika kwa kuiondosha Portugal ya Cristiano Ronaldo bao 1-0 na kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Shujaa wa Morocco ni Youssef En-Nesyri dakika ya 42 aliwanyanyua mashabiki wa Morocco na Waafrica kwa ujumla na kuandika historia mpya ya kutinga hatua hiyo.
Kwa ushindi huo Morocco wanasubiri mshindi kati ya Ufaransa na England mchezo utakaopigwa majira ya saa nne usiku.