Kocha mzambia, Honour Janza (62), amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuwatumikia Zesco United ‘wakata umeme’ ya Zambia kama Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo inayomilikiwa na Shirika la Imeme la Zambia.
Janza alikuwa kocha wa Namungo FC ya Lindi kabla ya kutoweka na kuelekea kwao Zambia kuwahi ‘deal’ hiyo. Haijajulikana ikiwa ataachana na Taifa Stars au ataendelea na jukumu hilo pamoja na kupata ajira hiyo mpya.
Zesco United ya Zambia imekuwa katika maboresha makubwa ya timu hiyo ambapo hivi karibuni walimrejesha kocha wao wa zamani George Lwandamina kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.