Mweyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan amepata kura 1914 huku akipata kura moja ya hapana.
Kwa Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania bara, Abdulrahman Kinana amepata kura 1,913 na mbili za hapana huku Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Dk.Hussein Ali Mwinyi amepata kura 1912 huku akipata kura tatu hapana.
WAJUMBE WA NEC TANZANIA BARA
WANAUME BARA
Igaga Mahenda(845), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa(720), Stephen Wasira(680), Mbunge wa Geita Joseph Musukuma(587), aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kaselela(574), Wambura Mwita(545), Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe(510), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye(508), Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima(497), Waziri wa Nishati Januari Makamba(452), Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Mwigulu Nchemba(450), aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya Anamringi Macha(435) na Dk.Ibrahim Msengi(415).
WANAWAKE BARA
Walioshinda wanawake ni Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Christina Mndeme(761), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angelina Mabula(770), Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk.Ashatu Kijaji(764), Hellen Makungu(755), aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Fenela Mukangara(747) na Waziri wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Angellah Kairuki(730).
WAJUMBE WA NEC ZANZIBAR
WANAUME ZANZIBAR
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof.Makame Mbarawa(798), Issa Haji Ussi(704), Joseph Abdalla Meza(701), Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka(698), Mohamed Said Mohamed(651), Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Hamza Khamis Chilo(637), Amin Salum Amour(610), Mohamed Habib Mohamed(583), Mbarouk Nassor Mbarouk(554), Abdulhafar Idrissa Juma(521), Nasir Ali Juma(419), Khamis Mbeto Khamis(416), Mbaraka Saidi Rashid(379), Abdullah Sadala Mabodi(363).
WANAWAKE ZANZIBAR
Dk.Saada Mkuya(653), Tabia Mwita(666), Najma Murtaza Giga(686), Leila Ngozi(702), Amina Hamis Omary (579) na Mvita Mustapha Ali(547).