Kiungo wa Yanga ambaye ni mchezaji bora wa Uganda kwa msimu uliopita, Khalid Aucho, amewataka mashabiki wa Yanga kuziba masikio na kuacha kusikiliza taarifa za uzushi kuhusu yeye. 

Aucho amepost picha yake katika ukurasa wake wa Instagram akiwa ameziba masikio na kuwataka mashabiki wake na familia ya Yanga kuacha kusikiliza taarifa za uzushi.  

Aucho ameandika hayo baada ya taarifa nyingi kuzagaa kwamba amekataa kuongeza mkataba na klabu yake ya Yanga ili akajiunge na klabu moja toka Falme za kiarabu. 

Mchezaji huyo kipenzi cha wanayanga amewasihi ‘wananchi’ kumakinika na michezo iliyoko mbele yao na kuachana na waandishi wanaotafuta umaarufu kupitia jina lake.