Bunge la Indonesia linatarajiwa kupitisha sheria ya uhalifu mwezi huu itakayowaadhibu watu wanaoshiriki ngononje ya ndoa kwa kifungo cha hadi mwaka mmoja.

Mwanasiasa nchini humo -Bambang Wuryanto, ambaye alihusika katika utungaji wa sheria hiyo, amesema kuwa inaweza kuidhinishwa wiki ijayo.

Iwapo sheria hiyo itapitishwa, itawaadhibu raia wa Indonesia pamoja na rai awa kigeni.

Adhabu hiyo ya uasherati inaweza kutekelezwa tu iwapo kuna watu watakaowasilisha malalamiko kwa mamlaka.

Kwa ambao wameoana, mmoja wao ana haki ya kuwasilisha malalamiko kama mshitakiwa ni mume au mke.

Sheria hiyo pia inawaruhusu wazazi wa ambao hawajaolewa kuwaripoti kwa kufanya ngono.

Kuishi kama mume na mke kabla ya ndoa pia kutapigwa marufuku na wale watakaopatikana na hatia wanaweza kukabiliwa na hukumu ya kifungo cha miezi sita jela.