Klabu ya Polisi Tanzania imemtangaza aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga kuwa kocha wake mpya baada ya mazungumzo ya muda mrefu na makubaliano ya pande zote mbili kufikiwa.
Kocha huyo mwenye uraia wa Congo na Ufaransa atakuwa na jukumu kubwa la kuisaidia timu hiyo kujinasua toka mkiani mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara.
Taarifa hiyo ya klabu ya Polisi yenye makazi yake Moshi, Kilimanjaro haijaeleza kocha huyo amesaini kandarasi ya miaka mingapi na wafunga buti hao.