Na Abel Paul,JamhuriMedia wa Jeshi la Polisi
Watuhumiwa wa vitendo vya ukatili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa mara wilaya ya Tarime kwa makosa ya kufanya ukeketaji na tohara kwa Watoto wa kike amabapo ni kinyume na sheria za nchi.
Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 2,2022 na msemaji wa jeshi la Polisi nchini Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime ambapo amebanisha kuwa katika siku za hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya watu wakihamasisha shughuli za ukeketaji kwa Watoto wakike katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.
Amebainisha kuwa tayati jeshi hilo linawashikiria watu kadhaa kwa tuma za kufanya vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike katika Wilaya ya Tarime ambapo ametoa wito kwa viongozi wa serikali za vijiji kuwa msatari wa mbele kukemea vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia.
Misime amebainisha kuwa Jeshi linaendelea na upelelezi na pindi upelelezi utakapo kamilka watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Aidha amesema kuwa jeshi hilo linawapa tahadhari wale wote wenye nia ya kufanya uhalifu mwisho mwa mwaka kwa kigezo cha kupata fedha ili washerehekee sikukuu za mwisho wa mwaka kuwa hawa salama na wasijaribu kufanya hivyo ambapo amebainisha kuwa Jeshi la Polisi liko makini na litawakamata wale wote wenye dhamira hiyo.
SACP Misime pia amesema katika siku za hivi karibu tumeshuhudia ajali za barabarani zikigharimu maisha ya watu ambapo amesema sheria na alama za barabarani zipo ambapo amewataka madereva kufuata sheria hizo ili kupunguza ajali kama sio kumaliza ajali.
Jeshi la Polisi nchini limetoa wito kwa wananchi na kutoa msisitizo kwa wananchi juu ya mambo ya kujiepusha na vitendo vya uhalifu wa kijinai na ajali za barabarani tunapoelekea mwisho wa mwaka 2022 katika maeneo mbalimbali hapa nchini na kusema Jeshi hilo halite sita kuchua hatu kali za kisheria kwa dereva yeyote atakaye sababisha ajali na kusema kuwa Jeshi hilo linaendelea kutimiza majukumu yake kila kona ya nchi na kuwaomba wananchi watoe taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi hilo.