Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesema kuwa imebaini uwepo wa baadhi ya taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila ya kuwa na leseni, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.
Aidha BoT imeahidi kuwahukulia hatua kali wanaofanya biashara ya kukopesha bila kuzingatia sheria huku ikiwataka wananchi kuepuka kukopa au kufanya kazi na taasisi, kampuni, au watu binafsi wambao hawana leseni.