Na Mussa Augustine,JamhuriMedia 

Naibu Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete, anatarijiwa kuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Chama Cha Wamiliki wa Matipa na Mitambo Tanzania ( TTMOA) Novemba 25 mwaka huu  Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa Chama hicho, Emmanuel Moshi wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amebainisha kwamba  uzinduzi huo utahudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo  maafisa waandamizi wa Serikali, vyama vya Sekta binafsi, Jumuiya ya wafanyabiashara na washirika maendeleo.

Amewaomba wamiliki wa Matipa na Mitambo kujiunga na  Chama hicho ili kufanya kazi kwa pamoja kukuza uchumi wa Taifa na kuongeza ajira kwa watanzania, na kuongeza kuwa chama hicho kimeendelea kukua na kwa sasa kina jumla ya wanachama zaidi ya 150 na kinafanya kazi ndani ya malengo yake.

Amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni kuunganisha, kuwakilisha na kutetea maslahi ya Jumuiya ya wamiliki wa matipa na mitambo nchini Tanzania, ambapo hiyo ni kupitia Sera, utetezi na ushawishi wanapofanya kazi na Serikali kwa niaba  ya wanachama wao.

Kwa upande wake, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya GF Trucks na Equipment, Smart Deus amesema kuwa kampuni hiyo iliamua kudhamini Chama hicho Ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwawezesha watanzania kupata ajira.

‘Tumeona kuwa wateja wetu wengi ni wanachama wa chama hiki, kwa hiyo ikatusukuma kudhamini  chama hiki kwa lengo la kukuza ajira, pili wateja wetu na kuhamisisha kuunga mkono juhudi za  ukuzaji wa Viwanda nchini”amesema Smart.Aidha, ameongeza kuwa, wanachama wao kuwepo katika chama hicho kinawarahisishia wao wanapokuwa na bidhaa mpya kuweza kuwafikia wateja wao kwa haraka  kwani wamekua na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wateja wao wanaponunua bidhaa