Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limepiga marufuku kitambaa cha “One Love” kwenye Kombe la Dunia 2022
linaloendelea nchini Qatar. Kitambaa hicho ni sehemu ya hamasa inayotumiwa na wanasoka wengi Ulaya hususani
manahodha kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja (ushoga) ambayo ni kinyume cha sheria na maadili katika mataifa mbalimbaliduniani.
Kwa mujibu wa taarifa za karibuni zimeeleza kuwa, shirikisho hilo la soka la kimataifa limesema marekebisho yoyote ya
nembo inayotumiwa na wachezaji uwanjani yanahitaji kibali chake.
Katika mkutano wenye mvutano kwenye Kombe la Dunia, FIFA ilijaribu kusuluhisha mzozo kati ya timu za Ulaya juu ya
matumizi ya kitambaa kisicho rasmi cha unahodha huko Qatar katika kampeni ya kupinga ubaguzi.
Uamuzi huo ulikuja saa chache baada ya nahodha wa Uingereza, Harry Kane na manahodha wengine kadhaa wa mataifa
mengine kusema kwamba, wangepuuza marufuku yoyote ya vitambaa vya upinde wa mvua vinavyotarajiwa.
Kane alivaa kitambaa cha “OneLove” kwa michezo miwili ya ligi iliyochezwa mwezi Septemba, lakini baraza linaloongoza
FA na Uingereza hawakuonesha onyo lolote.
FIFA inashinikiza mashirikisho saba ya soka ya Ulaya kufikiria upya kutoruhusu manahodha wao kuvaa vitambaa vya “One
Love”, ambavyo vina umbo la moyo, nembo ya rangi mbalimbali inayokusudiwa kutetea haki za mapenzi ya jinsia moja.
Aidha, FIFA ilijaribu kuwashawishi Wazungu katika mkutano wa hivi karibuni zaidi kuepukana na hamasa za namna hiyo
badala yake vitambaa vinaweza kutumika kutoa jumbe kama “Kandanda inaunganisha Ulimwengu” na “Shiriki Lishe
Kamili,” kati ya jumbe zingine za kijamii ambazo zilipaswa kukuzwa na vitambaa zilizopendekezwa na FIFA, kulingana na
taarifa kutoka FIFA.
Baraza linaloongoza sasa linatofautiana na makundi kama Ujerumani, ambayo nahodha wake Manuel Neuer alisema
ataendelea kuvaa kitambaa cha “OneLove”.
“Mataifa mengine ya Ulaya yamevaa (kitambaa) na ni vizuri tunafanya hivyo pamoja,” Neuer alisema Jumamosi.
Christian Eriksen wa Denmark alisema kuwa bila kujali vikwazo vyovyote vya FIFA, nahodha wa taifa lake Simon Kjaer
pia atakuwa akivaa kitambaa cha upinde wa mvua.
“Sisi kama nchi tunavaa, nahodha wetu atakuwa amevaa kitambaa cha OneLove,” Eriksen alisema. “Matokeo yatakuwaje
sijui, lakini tutaona.”
Zaidi ya hayo, kuna uvumi kuwa FA ya Uingereza tayari inaunga mkono kampeni ya “OneLove” bila kujali na kuuliza
ufafanuzi kuhusu utangamano wa FIFA na vitambaa vya upinde wa mvua.
Tangu kupata haki ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2010, Qatar imekuwa chini ya uangalizi mkubwa wa kimataifa
kuhusu haki za binadamu na masuala ya mapenzi ya jinsia moja.
Hata hivyo, mtendaji mkuu wa Qatar 2022 Nasser al Khater amesema serikali haitabadilisha sheria zake kuhusu mapenzi ya jinsia moja, na kuwataka wageni kuheshimu utamaduni wao.