Na Abel Paul,JamhuriMedia-Jeshi la Polisi
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu wa Polisi SP Solomon Mwangamilo amewataka madereva kuwa makini katika matumizi ya vyombo hivyo pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara.
Hayo yamesema leo Novemba 8, 2022, wakati wa kukabidhi pikipiki kwa viongozi wa dini kutoka Manyara,Kilimanjaro pamoja na Arusha ambapo amesema kuwa viongozi wanaowajibu wa kutibu mionyo ya wanadamu kiroho ambapo amewaomba kutokubali kuvutwa na shetani wakati wa matumizi ya vyombo hivyo.
SP Solomon amesema wao kama Jeshi la Polisi wanawajibu kutoa elimu kwa makundi yote ili kuwa na uelewa wa pamoja ili kukomesha ajali katika mkoa wa wa Arusha.
Kwa upande wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dkt. Barnabs Mtokambali amesema lengo la kutoa vyombo hivyo ni kuwafikia waamini wa dhehebu hilo na kutoa huduma ya kiroho na kazi za kanisa ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya maendeleo ya kanisa hilo.
Wakati huo huo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, SP Mwangamilo amewata madereva wa vyombo vya moto maarufu mando wanaofanya safari zao nje ya jiji la Arusha na kwenda maeneo ya vijijini kufanya marekebisho ya vyombo hivyo ili kupunguza ajali. .
Ametoa kauli katika Kata ya Meserani Wilaya ya Monduli alipokuwa akizungumza na maderva wa vyombo hivyo ambapo amewataka kufanya marekebisho na kufuata sheria za usalama barabarani.