Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea asubuhi leo katika ziwa Victoria wakati ikitua imeongezeka na kufikia vifo vya watu 19.
Chalamila ametoa taarifa hiyo leo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika eneo la tukio Bukoba.
“Katika majeruhi 26 waliookolewa mwanzoni hakuna aliyefariki, tukaendelea kuokoa wengine kwa kushirikiana na vyombo vya dola, wenzetu wa Redcross na magari ya watu binafsi hivyo tumesaidia kuivuta ndege pale ilipokuwa hadi hapa iliposogea.
“Hivi punde tumefanikiwa kuopoa miili ya watu 19 ukijumlisha na majeruhi 26 na vifo 19 inakuwa 45 na sio 43 kwa taarifa iliyotolewa awali,’ amesema.
Chalamila amesema kuwa katika shughuli za uokoaji kuna wengine walikuwa wanakwenda chini hivyo bado wanaendelea kujiridhisha kama ni idadi halisi ya abiria au ilikuwa zaidi ya hapo.
Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Issessanda Kaniki amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu watatu kabla ya Majaliwa kufika na kutangaza idadi ya waliokufa kuwa ni 19.
Ndege hiyo ya Precision Air ambayo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba.
Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu kwa habari