Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia
Rais Samia ameridhia Watumishi walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti kurejeshewa michango yao waliyochangiwa katika Mifuko ya Hifadhi ambayo kwa PSSSF ni asilimia tano na Kwa NSSF ni asilimia kumi ya mshahara.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Oktoba 26,2022,
Amesema marejesho ya michango yataanza rasmi kutolewa Novemba Mosi, 2022 na amezitaka mamlaka husika kukamilisha malipo hayo kwa haraka zaidi.
“Marejesho ya michango kwa watumishi hao yataanza kufanyika kuanzia tarehe 1, Novemba, 2022 na tungependa kwa kweli jambo hili likamilike ndani ya muda mfupi kwa hiyo ili kuwezesha malipo hayo kufanyika mtumishi husika atatkiwa kwenda kwa aliyekuwa mwajiri naomba wasiamkie kwenye Mifuko ya jami.”amesema.
Aidha Prof.Ndalichako amewataka watumishi hao kufuata utaratibu wa kudai stahiki zao na kusisitiza kuwa malipo hayatafanyika kwa pesa taslimu bali kwa njia ya kibenki.
“Taratibu ni zilezile anatakiwa aliyekuwa mwajiri wake akiwa na nyaraka zifuatazo awe na picha mbili pasaport size awe na nakala za kibenki yaani kwenye akaunti iliyo hai malipo haya hayatolewi pesa taslimu yatafanyika kwenye benki kwa hiyo lazima mtumishi husika aonyeshe taarifa zake za kibenki lakini pia atatakiwa awe na kitambulisho” amesema.