Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumatatu, Oktoba 24, 2022) amewasili Seoul, Jamhuri ya Korea Kusini kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.

Majaliwa alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Togolani Mavura pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi katika nchi hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipokea maua kutoka kwa watoto Neviah Mwamlima   (kushoto) na  Bradley Massawe wakati  walipowasili kwenye hoteli ya Lotte  iliyopo Seoul nchini Korea ya Kusini, Oktoba 24, 2022  kuanza ziara ya kikazi nchini humo.  Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini humo,  Mhe. Togolani Mavura. 

Kesho (Jumanne, Oktoba 25, 2022) Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea kkampuni ya kutengeneza mabehewa na injini za treni cha SRT kilichopo katika mji wa viwanda wa Mungyeong pamoja na kituo cha ubunifu kilichopo Pangyo.

Aidha, akiwa Korea Kusini, Waziri Mkuu anatarajiwa kushiriki kongamano la biashara na kukutana na wamiliki wa makampuni makubwa na wenye viwanda. Vilevile, atakutana na Watanzania waishio Korea Kusini.

Waziri Mkuu, Kassim. Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakisalimiana na baadhi ya Wwatanzania waishio  nchini Korea ya Kusini waakati walipowasili kwenye hoteli ya Lotte iliyopo Seoul nchini humo  Oktoba 24, 2022 kwa ziara ya kikazi .

Kupitia vikao hivyo, Tanzania inatarajiwa kuimarisha mahusiano na Korea Kusini ambayo yamedumu kwa miaka 30. Vilevile, kukuza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji, kuangalia fursa za kukuza uchumi wa bluu, utalii, mahusiano ya anga na ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na utamaduni.