nmb-4Washington Dulles – American 77

 

Umbali mrefu wa Kusini Magharibi mwa Boston, viunga vya Virginia, Washington DC zaidi ya wanaume watano walikuwa wakijiandaa kupanda ndege saa 1:15 asubuhi. Miongoni mwao walikuwako Khalid Al Mihdhar na Majed Moqed. Walikaguliwa, ikakaguliwa mizigo yao na tiketi zao za Ndege 77 iliyokuwa ikielekea Los Angeles ambako ndani ya dakika 20 nyingine walikuja pia Hani Honjour na vijana wawili Nawaf Al Hazmi na Salem Al Hazmi.

Hani Hanjour, Khalid Al Mihdhar na Majed Moqed walikuwa na nembo ya CAPPS. Walikuwa na nembo hizo kwa sababu wale ndugu hawakuwa na picha ya utambulisho wala hawakuweza kuzungumza vema Kiingereza na kwa vile wakala yule alibaini wasafiri wale wawili walikuwa na dukuduku, njia pekee iliyokuwa salama ilikuwa ni mizigo yao kuwa pale kwa uthibitisho vingefanyika ya kuwa wameshapanda ndege tayari.

Watekaji wote watano walipitia katika vizuizi cha ulinzi cha Magharibi. Vizuizi vilikuwa vimezungushiwa ving’amuzi vya TV (Closed Circuit Television) ambavyo vilikuwa vikirekodi matukio yote ya wasafiri. Mnamo saa 1:18 Mihidhar na Moqed waliingia katika ukaguzi na kupita.

Mihidhar na Moqed waliweka mizigo yao katika mkanda wa kumulikwa chini ya mionzi ya X-ray. Dakika 20 baadaye yaani saa 1:35 msafiri mwingine wa ndege ya America 77, Hani Hanjour aliweka mabegi yake mawili katika mkanda wa X-Ray katika kizuizi cha Magharibi (Main Terminal) na akaendelea na mchakato ule bila king’ora (alarm), baadaye Nawaf na Salem Al Hazmi waliingia pia katika kukaguliwa.

Salem Al Hazmi alifanya uchunguzi wa kifaa kijulikanacho kama kinasa chuma na aliruhusiwa. Nawaf Al Hazmi alizima king’ora na vinasa chuma Na. 1 na 2 havikunasa na walitiliwa shaka kabla hawajavuka. Na zaidi ya hapo kibegi chake cha mgongoni kilimulikwa na kifaa kijulikanacho kama Explosive trace detector (kifaa kigunduacho vitu mbalimbali vya mlipoko. Mwenendo wa video unaonesha kuwa alikuwa amebeba kitu kisichojulikana katika mfuko wake wa nyuma.

 

Newark – United 93

Kati ya saa 1:03 na 1:39 asubuhi, Saed Al Ghamdi, Ahmed Al Nami, Ahmad Al Haznawi na Ziad Jerrah walikaguliwa katika kaunta ya United Airlines kwa ajili ya kupanda ndege 93 kuelekea Los Angeles. Wawili walikaguliwa mabegi, wawili hawakukaguliwa. Haznawi alichekechwa kwa kifaa cha CAPPS. Begi lake lilichunguzwa kwa ukaribu zaidi kubaini kama kuna vitu vyenye mlipuko hatari na baadaye kupakiwa ndani ya ndege.

Wanaume hao wanne walipitia katika vizuizi vya ulinzi vilivomilikiwa na United Airlines na kufanya kazi chini ya Mkataba wa Argenbright Security kama vizuizi vya ulinzi vilivyokuwa Boston vilipungukiwa televisheni (Circuit Television), hivyo basi hakuna ushahidi waki – documentary kuonesha namna gani watekaji walipita kwenye zile check pints.

Wanaume wale wanne walipanda ndege kati ya 1:39 na 1:48 wote hawa walikuwa wa viti vya Cabin ya kwanza. Ndege yao haikuwa na Business-class, Jerrah alikuwa na 1B, Nami 3C, Ghamdi 3D na Hznawi 6B.

 

Utekaji wa Ndege – American 11

Ndege American Airlines Na. 11 ilikuwa ikitoa huduma isiyotua mahala (non-stop service) kutoka Boston hadi Los Angeles. Mnamo Septemba 11, Rubani John Ogonowski na Ofisa namba moja, Thomas Mc Guiness alikuwa rubani wa Boeing 767. Ndege ilibeba wahudumu tisa ikiwa ndiyo idadi inayotakiwa, wasafiri 81walipanda ile ndege wakiwemo wale magaidi watano.

Ndege iliondoka saa 1:59 kabla ya saa 2:14 ilikuwa imekwea umbali wa futi 26,000 mawasiliano yote pamoja na takwimu za mambo ya anga vilikuwa sawa. Katika kipindi kile saini ya mkanda wa mashariki ilipaswa kuwa imegeuzwa ili wahudumu waanze kutoa huduma za cabin.

Wakati ule, American 11 ilikuwa na utaratibu wake wa mwisho wa mawasiliano na usawa wa ardhi baada ya kuwa imepata maagizo ya uvukaji (navigational instructions) kutoka kituo cha Air traffic control cha Boston sekunde 16 baada ya mawasiliano yale, ATC ilimwagiza rubani akwee hadi futi 35,000. Ujumbe ule pamoja na majaribio yote ya kuwasiliana na ndege hayabainishwi, inaaminika utekaji ulianza saa 2:14 au muda mfupi baada ya pale.

Ripoti kutoka kwa wahudumu wa ndege katika kochi la cabin Betty Ong na Madeline, zinatueleza mengi juu ya namna utekaji ulivyotokea. Ulipoanza baadhi ya watekaji hasa Wai Al Shehri na Waleed Al Shehri waliokuwa wamekaa mstari wa pili daraja la kwanza. Waliowachoma visu wahudumu wawili wa ndege ambao hawakuwa na kinga yeyote kipindi ambacho walipaswa kuanza kujiandaa kutoa huduma ya cabin.

“Hatujui kwa hakika ni kwa namna gani watekaji walipata mpenyo wa kuinglia kwenye cockpit – yaani chumba cha rubani. Kanuni za F.A.A zinataka milango iwe imefungwa wakati ndege ikiwa angani. Ong anawazua ya kwamba watekaji walikuwa wameuhadaa mfumo mzima. Pengine magaidi waliwachoma visu wahudumu na kuchukua ufunguo wa cockpit na kumlazimisha mmoja wao kufungua mlango wa cockpit au kumhadaa captain au Ofisa namba 1 au wahudumu walikuwa wamejisahau.

Muda mchache baadaye, Atta gaidi pekee ambaye alikuwa ndani ya ile ndege mwenye mafunzo ya kuendesha ndege, alipata wasaa wa kuingia kwenye cockpit kutoka kiti cha business class na kwa uwezekano mkubwa akipewa ushirikiano na Omari.

Wakati tukio hili lilijiri msafiri Daniel Lewin aliyekuwa amekaa jirani na Atta na Omari alichomwa kisu na moja ya watekaji, pengine Satam al Suqami aliyekuwa amekaa pembeni mwa Lewin. Lewin alikuwa ametumikia miaka minne katika jeshi la Israel; kuna uwezekano alitumia uzoefu wake kuwazuia watekaji wale mbele yake bila kujua mwingine alikuwa kandoni mwake.

Mapema watekaji wakawa na udhibiti madhubuti wa ndege ile wakinyunyiza upupu, maji ya pilipili na vitu vingine vyenye kusababisha maumivu makali kwenye daraja la kwanza ili kuwalazimisha wasafiri na wahudumu wa ndege waondoke katika nafasi zao walidai wanabomu.

Baada ya dakika tano za utekaji huo kuanza, Betty Ong aliwasiliana na American Airlines – Southern Reservation Office Cary North Caroline kupitia AT & T airphone kuripoti dharula ile.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza hapo Septemba 11 ambako wahudumu wa ndege walichukua hatua nadra nje ya uwigo wa mafunzo yao ambayo yalisisitiza kwamba wakati wa utekaji walipaswa kuwasiliana na marubani wa ndege. Simu hiyo ya dharura ya Ong ilidumu kwa muda wa dakika 25 akitolea ufafanuzi wa tukio lile.

Mnamo saa 2:19 hivi, Ong aliripoti ya kuwa chumba cha rubani hakitoi majibu, lazima kuna mtu amechomwa kisu katika business class na ninadhani kuna hewa ya sumu huwezi pumua sijui nadhani tumetekwa.”

Saa 2:21, moja ya wafanyakazi wa Marekani akipokea simu ya Ong kule North Carolina, Nydia Gonzales alitaarifu kituo cha operesheni cha American Airlinesa Fort Worth, Texas habari zile zikimfikia Craig Marquiz – Maneja wa zamu.

Mapema, Marquiz alibaini kuwa hii ilikuwa ni dharau na kuziagiza mamlaka zichukue tahadhari. Mnamo saa 2:23 mawasiliano ya kumpata rubani yaligonga mwamba. Dakika sita baadaye mtaalamau wa mawasiliano ya anga wa American Airlines aliwasiliana na kituo cha F.A.A Boston, kituo kilikuwa na hadhari ya tatizo lile.

Kituo cha Boston kilijua tatizo la lile ndege kwa sababu punde tu kabla ya saa 2:25 watekaji walikuwa wamefanya majaribio ya kuwasiliana na wasafiri. Simu ilikuwa imewekwa kiwambo (Keyed) na mapema moja ya watekaji walisema, “Haukuna mtu kujongea kila kitu kitakuwa shwari ukijaribu kufanya mjongeo wa aina yeyote utahatarisha masiha yako na ya ndege kwa ujumla… ni suala la kutulia.”

Wadhibiti wa mawasiliano ya anga walipata fununu ile; Ong hakufanikiwa.

Watekaji inawezekana hawakujua kuendesha mfumo wa mawasiliano wa chumba cha rubani kwa ufasaha. Kati ya saa 2:25 na 2:29 Amy Sweeney alijaribu kufanya mawasiliano na American Flight Service – Boston, lakini mawasiliano yale yalikatizwa baada ya kuripoti kuwa moja ya wasafiri alikuwa ameumizwa vibaya ndani ya ndege. Dakika tatu baadaye, Sweeney aliunganishwa tena na kuanza kutoa habari kwa meneja Michael Woodward.

Mnamo saa 2:26, Ong aliripoti ya kwamba ndege imepoteza mwelekeo, ilikuwa ikipaa shaghala baghala. Dakika moja baadeye ndege 11 ilirudi kusini. Walianza pia kupata vitambulisho vya watekaji kwa vile Ong na Sweeney walipitia viti namba za wale watekaji wa kuingia kwenye chumba cha rubani.

Sweeney aliripoti katika hali ya utaratibu kabisa kuwa ndege ilikuwa imetekwa. Msafiri mmoja ndani ya daraja la kwanza alikuwa amekatwa koromeo, wahudumu wawili wa ndege wamechomwa visu mmoja akiwa akipumua kwa msaada wa gesi ya oksijeni. Sweeney alimwambia Woodward kuwa yeye na Ong walikuwa wakijitahidi kwa hali na mali kutoa taarifa kwa watu walio chini ya ardhi.

Mnamo saa 2:38, Ong alimwambia Gonzalez tena katika mida hii, ndipo alipomwambia Woodward ya kuwa watekaji walikuwa ni raia wa Mashariki ya mbali, mmoja alikuwa akizungumza kiingereza kidogo, na mwingine akibonga umombo murua! Watekaji wamejipenyeza hadi kwenye chumba cha rubani na hujui imetokea vipi.

Mnamo saa 2:40, kituo cha oparesheni cha America walimwambia Marquiz ya kuwa trafiki Controller walikuwa wametangaza ndege 11 ilikuwa imetekwa.

Mnamo saa 2:44, Gonzalez aliripoti kupotea mawasiliano na Ong wakati huohuo Sweeney aliripoti kwa Woodward kuwa “kuna jambo baya” tuko katika mwendo mkali Woodward alimtaka Sweeney kuangalia nje ya dirisha kuangalia kama angeweza kutathmini wako wapi Sweeney alijibu, “Ndege inaanza kupaa mwelekeo wa chini – chini sana – Sekunde chache baadaye akasema; “Mungu wangu – tunaelekea chini kabisa.”

Simu ikakatika mnamo saa 2:46, American 11 ilikuwa imebamizwa katika jengo pacha la World Trade Centre, New York City. Wote waliokuwa ndani ya ndege kujumlisha na idadi isiyojulikana ya watu waliokuwa katika jingo lile wote waliuawa palepale.

 

>>ITAENDELEA

O784 142 137