Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar, akizungumzia mafanikio ya ziara yake ya Kikazi Nchini Oman, mazungumzo hayo yualiofanyika katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, (kulia kwa Rais)Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzinar Hemed Suleiman Abdulla na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohammed. (Picha na Ikulu)
Rais S wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuelezea mafanikio ya ziara yake ya Kikazi ya siku nne Nchini Oman
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, jana usiku akitokea nchini Oman baada ya kumaliza ziara yake ya Kikazi ya Siku Nne Nchini humo.(Picha na Ikulu)