Na Stella Aron, JamhuriMedia, Dar
Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya, William Ruto wamekubaliana kuondoa vikwazo 54 kati ya 68 ambavyo vilikuwa vikichangia kukwamisha biashara kati ya nchi hizo.
leo Jumatatu Oktoba 10, 2022 Ikulu Dar es Salaam ikiwa ni miongoni mwa mambo waliyojadiliana kutafutiwa ufumbuzi wa haraka kwa maslahi ya pande zote mbili.
Rais Samia amesema kuwa kulikuwa na vikwazo 68 vilivyokuwa vikikwamisha kufanyika kwa biashara na tayari vikwazo 54 vimeondolewa na kubaki vikwazo 14 ambavyo navyo vitaondolewa mara baada ya mawaziri wa nchi hizo pamoja na wataalam mbalimbali kukutana haraka.
“Tumewataka mawaziri wetu wakutane haraka na kufanyia kazi vikwazo hivyo ili kuwe na uhuru wa kibiashara kwani kazi hii ilianza na Rais Mstaafu, Uhuru Kenyata na tulikubaliana kwa kuwataka wataalamu wetu kufanyia kazi vikwazo vya biashara vilipo.
“Mawaziri hao walitambua vikwazo 68 na vilifanyiwa kazi 54 na
Rais Samia amesema ziara ya Ruto inatoa fursa ya kutathimini fursa ya ushirikiano katika ngazi zote,” amesema Rais Samia.
Rai Samia amesema kuwa katika majadiliano hayo yamezungumzia sekta mbalimbali kama kumarisha kwa biashara, kujenga ushirikiano, kuimarisha ulinzi kwenye mipaka ya nchi hizo mbili,kusimamia suala la usafirishaji dawa za kulevya,ujangili, usafirishaji watu.
“Tumekuwa tukipata sifa mbaya duniani ya usafirishaji binadamu na Kenya hivyo hivyo hivyo ni vizuri wahusika wanaojihusiaha na biashara hiyo wakashughulikiwa,” amesema.
Rais Samia amesema kuwa katika kutafuta maendeleo kwa Tanzania na Kenya hakuna sababu ya kugawana umaskini kwani wote tuna lengo la kuimarisha ushirikiano na kupata maendeleo.
“Hatuna sababu ya kugawana umasikini kwa Tanzania na Kenya na udhalili lakini tugawane utajiri tutakaofanya kupitia biashara,” amesema Rais Samia.
Naye Rais wa Kenya, Willam Ruto amesema Serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania akibainisha kwamba, kuondoshwa kwa changamoto hizo kumeinufaisha zaidi Tanzania ikilinganishwa na Kenya.
Amesema biashara baina ya Tanzania na Kenya imezidi kuimarika ambapo usafirishaji wa bidha kwa mwaka mmoja imepanda kutoka bil.27 kutoka Tanzania kufikia Sh.bil.50 kwenda Kenya.
Amesema kuwa kwa upande wa Kenya usafirishaji wa bidhaa kutoka Kenya kuja Tanzania umepanda kutoka Sh.bilioni 31 kufikia Sh.bilioni 45.
Amesema kuwa hivi sasa Kenya inanunua vitu vingi kutoka Tanzania kuliko wanavyonunua kutoka Kenya na hii ni kutokana na ushirikiano baina ya nchi hizo.
Hata hivyo Rais Ruto ameungana na kauli ya Rais Samia ya kuwataka Mawaziri baina ya Kenya na Tanzania kufanyia kazi haraka changamoto zilizobaki ili kufikia mwishoni mwa mwaka huu changamoto zote hizo ziwe zimetatuliwa.
Rais Ruto yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo aliwasili jana na leo kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan na kufanya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam