Shani Suleiman (35),mkazi wa Morogoro Mjini amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka 12.
Hukumu hiyo imetolewa Septemba 28, 2022 katika Mahakaka ya Rufani Tanzania baada ya mahakama kuthibitisha bila mashaka licha ya mtumiwa kukata rufaa.
Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Rufani Tanzania jijini Dar es Salaam na jopo la majaji watatu,Mary Levira,Stella Mugasha na Abrahaman Mwampashi, ilitupilia mbali rufaa ya mfungwa huyo.
Hii ilikuwa rufaa ya pili kutupwa baada ya ile ya kwanza ya kupinga hukumu ya kifungo cha maisha jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro 2019 kutupwa na Jaji Joaquine De-Mello wa Mahakama Kuu, Julai 28, 2021.
Ushahidi umeonyesha mwanamke huyo alikamatwa baada ya mama mzazi wa mtoto huyo, akiwa na rafiki yake, kuweka mtego katika nyumba ya mwanamke huyo na kurekodi tukio hilo kwa kutumia simu janja.
Hatua hiyo imetokana na baada ya mtoto kumweleza mama yake kuwa mtuhumiwa ambaye ni maarudu kwa jina Mama Shafii amekuwa akimwambia amwingilie mara kwa mara na wakati mwingine kinyume cha maumbile na mchezo huo aliufanya kwa miaka mitatu hadi mwaka 2019.