“Mwanadamu anapaswa kumaliza vita, vinginevyo vita itammaliza mwanadamu.”

Haya ni maneno ya Rais wa 35 wa Marekani aliyeuawa mwaka 1963. John F. Kenney alikuwa akiamini kuwa dunia inaweza kuwa salama zaidi kwa kutoendekeza vita.

Clinton: Tusiisahau jamii

“Hebu tubebe jukumu pana, si kwa ajili yetu na familia zetu tu, bali kwa ajili ya jumuiya na nchi yetu.”

Haya ni maneno ya Rais wa 42 wa Marekani, Bill Clinton. Clinton alikuwa mmoja wa marais wa Marekani walioonyesha upendo mkubwa kwa Afrika.

Jefferson: Wamarekani wangejua!

“Mungu wangu! Ni kwa kiwango kidogo kiasi gani watu wa taifa langu [Wamarekani] wanafahamu baraka walizojaliwa, ambazo hakuna watu wengine wenye kuzipata!”

Haya ni maneno ya Rais wa tatu wa Marekani, Thomas Jefferson, aliyeshiriki kuandika Katiba ya Marekani mwaka 1776.

Luther King Jr.: Rafiki wa kweli

“Mwisho wa siku [baada ya harakati] hatutakumbuka maneno ya maadui zetu, bali ukimya wa marafiki zetu.”

Haya ni Maneno ya Dk. Martin Luther King, Junior aliyeishi kati ya Januari 15, 1929  na Aprili 4, 1968. Alikuwa Mchungaji wa Kibaptisti na mwanaharakati mpigania haki za binadamu mashuhuri kutoka Marekani.