Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Dar
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetangaza kuanza kugawa gawio la Tshs 1.5 bilioni kwa Wateja, Mawakala na Wadau kutokana na matumizi yao ya huduma ya Airtel Money .
Akizungumza leo Septemba 22,2022 jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza kuanza kutoa gawio la faida hiyo hiyo, Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Isack Nchunda amesema kuwa “gawio hili litatolewa kwa Wateja, Mawakala na wadau ambao wamekuwa wakitumia huduma za Airtel Money kwa kipindi cha Aprili mpaka Juni 2022’’.
Airtel imekuwa ikitoa Gawio hili kwa Wateja, Mawakala na Wadau wa Airtel Money tangu 2015. Airtel inagawa gawio lake kwa wateja na mawakala wa Airtel Money kulingana na matumizi yao ya Airtel Money kwa kila siku kwenye kila robo ya mwaka.
Nchunda amesema kuwa “wateja wanaweza kutoa kiasi cha gawio lake analopata akuaamua kutumia kwa kununua bando au muda wa maongezi, kulipia bili mbali mbali au kufanya miamala kwa kuwatumia wanafamilia, marafiki au kuongeza mtaji kwenye biashara zao, mbali na gawio hilo bado wateja wetu watandelea kufaidi kutuma na kutoa pesa bila tozo za serikali kwa kiasi cha mpaka Tshs 29,999 kwani Airtel Money inakulipia tozo hizo”’.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Beatrice Singano alisema kuwa kila Mteja, Wakala au Mdau wa Airtel Money ataanza kupokea gawio lake kuanzia kupitia akaunti yake ya Airtel Money.
‘Mawakala wetu pia watapokea faida yao kwa kupitia akaunti zao za Airtel Money kama ilivyo kawaida. Natoa rai kwa mawakala wetu kuendelea kutoa huduma iliyo bora kwa wateja wetu nchini kote kwani kwa kufanya hivyo kunatoa nafasi ya kuendelea kupata gawio kwa kila robo ya mwaka’ amesema Singano.
‘Naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza wateja wetu, mawakala na
wadau kwa kuendelea kutuamini na kutumia huduma zetu za Airtel Monay ambazo ni salama, nafuu na za haraka,’ ameongeza Singano.