Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kupitia wakili wake George Murugu imesema kuwa ilitangaza kwa ‘haraka’ matokeo ya Urais kufuatia wasiwasi wa usalama wa wafanyikazi wake.
Amesema tume hiyo ilifanya uamuzi wa kutotangaza majimbo 27 yaliyosalia licha ya kujumlishwa na kuthibitishwa.
Amesema matokeo yalikuwa tayari kwa kutangazwa na Profesa Abdi Guliye lakini kutokana na tishio lililokuwa likijitokeza, walichagua kutangaza matokeo ya urais pekee.
Murugu aliongeza kuwa unyanyasaji wa mara kwa mara ambao wafanyakazi wa tume hiyo walikuwa wakikabiliana nao ambao ni pamoja na kukamatwa na vitisho ndio ulisababisha uamuzi huo.
“Yeye alizingatia kuhusu usalama wa wafanyikazi wake ambao wakati huo walikuwa wakikabiliwa na kukamatwa, kutekwa nyara na kujeruhiwa kwa maafisa wakiwemo makamishna,” amesema.
Murugu alikuwa akijibu swali kutoka kwa majaji wa mahakama ya juu kuhusu ni kwanini waliharakisha kutangaza matokeo bila kujumlisha matokeo mengine ambayo tayari yalikuwa yamethibitishwa