Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema kuwa serikali imeandaa mpango wa kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kuwapatia mitaji ili waweze kuboresha shughuli zao

Hayo ameyasea leo Agosti 30,2022 wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya wizara ya mifugo na uvuvi (sekta ya uvuvi) na benki ya maendeleo ya kilimo tanzania – TADB, hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki,akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) hafla iliyofanya leo Agosti 30,2022 Jijini Dodoma.

Mpango huu ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani katika hotuba yake aliyoitoa tarehe 07.01.2022 katika kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisisitiza kutumika kwa fursa zilizopo katika kukuza Uchumi wa Buluu ikiwemo uvuvi na ukuzaji viumbe maji.

Aidha, wakati akifunga Maonesho ya Sherehe za Wakulima (NANENANE), Mheshimiwa Rais aliagiza Wizara kuhakikisha kuwa uzalishaji wa Samaki unaongezeka kutoka tani 497,567 na kufikia tani 600,000 ifikapo mwaka 2025.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Tanzania, Frank Nyabudenge (wa pili kulia wakisaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) hafla iliyofanyika leo Agosti 30,2022 Jijini Dodoma.

”Katika utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeandaa Mpango wa kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa vyama vya ushirika, vikundi vya wavuvi, wakuzaji viumbe maji, wavuvi binafsi na makampuni ya wavuvi.”amesema Waziri Ndaki

Hata hivyo amesema kuwa Mikopo hiyo itahusisha zana za kisasa za uvuvi ikiwemo boti, nyavu, injini, vizimba, vifaranga vya samaki, chakula cha samaki na pembejeo za ukulima wa mwani.

Waziri Ndaki ametoa wito kwa wavuvi na wakuzaji viumbe maji kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo ili iweze kuwanufaisha,pia amezisihi Halmashauri katika maeneo ya mradi kwenda kuwahamasisha wananchi wake ili waweze kuitumia kuitumia fursa hii ipasavyo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega,akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.

Aidha, Waziri Ndakiamemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha shilingi bilioni 60 kwa ajili ya kuendeleza Sekta ya Uvuvi, fedha ambazo zipo katika bajeti ya mwaka 2022/2023.

”Endapo Fedha tulizopewa shilingi bilioni 60 zikitumika vizuri upo uwezekano mwaka ujao wa fedha hizo zikaongezeka.”amesema

Waziri Ndaki amesema kama viongozi watahakikisha wanawasimamia wataalam wa Wizara kwa kuwa mradi huu unatakiwa kutakelezwa kwa muda maalum, hivyo ifikapo Juni 30, 2023 utekelezaji wa mradi huu uwe umekamilika.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa kasi ya utoaji mikopo kwa wavuvi kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo ni ndogo, kwani mahitaji ya watanzani, kasi ya kuwafiki na urahisi wa upataji mikopo bado ni mdogo.

”TADB inayo kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha kwamba mikopo inafika kwa walengwa, kwani watu wengi wamehangaika kupata mikopo hasa wavuvi wadogo na kusababisha kukata tamaa na kuacha kufanya shughuli za uvuvi.”amesema Ulega

Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Frank Nyabudenge,akielezea jinsi walivyoamua kutoa Mikopo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) hafla iliyofanyika leo Agosti 30,2022 Jijini Dodoma.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma amesema kuwa Kamati imefurahishwa sana na mpango wa serikali wa kutoa mikopo isiyo na riba inayokwenda kuwasaidia wavuvi na wakuzaji viumbe maji. Mradi huu utakwenda kusaidia kuongeza uzalishaji wa samaki utakaokwenda kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo.

Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah amesema kuwa boti hizo zina urefu wa mita 7 hadi 14 zikiwa na injini zenye uwezo wa nguvu za farasi 9.9 hadi 60. Pia boti hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba wavuvi 6 – 20, kubeba Samaki tani 1.5, mtambo wa kufuatilia/kutambua uwepo wa Samaki (Fish finder), kifaa cha kuongoza boti (GPS), vifaa vya kuokolea Maisha na zana za uvuvi zikijumuisha mishipi na nyavu. Jumla ya shilingi Bilioni 11.5 zimetengwa kwa ajili ya kukopeshwa na mkopo huo utalipwa kwa muda wa miaka mitano (5) bila Riba.

Wizara pia itatoa mkopo kwa Wafugaji Samaki kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kujenga jumla ya vizimba 831 ambapo kila kizimba kimoja kitakuwa na ukubwa wa mita za ujazo 144 M3 – 256 M3. Vilevile, itatoa jumla ya vifaranga 4,080,000 na chakula cha Samaki tani 3,482.5.

Naibu Katibu Mkuu, OR TAMISEMI (Afya), Dkt. Grace Magembe ,akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) hafla iliyofanyika leo Agosti 30,2022 Jijini Dodoma.

Aidha, mkataba huo uliosainiwa leo utahusisha wakulima wa mwani ambapo jumla ya wakulima 821 watakopeshwa kamba 108,372, tai tai 7,152,552 pamoja na mbegu za mwani. Kwa ujumla kiasi cha shilingi Bilioni 21 zitatumika kwa ajili ya vizimba na zao la mwani.

Awali Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Frank Nyabudenge amesema kuwa benki hiyo ni taasisi ya kifedha ambayo ni benki ya serikali iliyojikita kwenye sekta ya kilimo. Moja ya malengo makubwa ya kuanzishwa kwake ni kuchangia utoshelevu wa chakula na usalama endelevu wa chakula nchini ambapo ni pamoja na utoaji lishe bora.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb) akitoa salam za kamati wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) hafla iliyofanyika leo Agosti 30,2022 Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, OR TAMISEMI (Afya), Dkt. Grace Magembe amemuhakikishia Waziri kuwa TAMISEMI itashiriki kikamilifu kwenye mkakati huo kwa kuwa tayari wanayo mifumo ambayo ilikuwa ikitumika kwenye utoaji wa fedha. Hivyo watashirikiana na wataalam kutoka Sekta ya Uvuvi kuangalia ni wapi wanafanya vizuri na kama kutakuwa na changamoto ziweze kutatuliwa ili mradi huu uweze kuleta tija na matokeo yaliyotarajiwa.