Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema wakati alipofika Nyumbani kwa Marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Agosti 2022. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Bi. Doreen Kimbi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema wakati alipofika kutoa pole nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiongoza sala ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP)  marehemu Augustine Lyatonga Mrema walipofika msibani nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Agosti 2022