Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi ametoa maelekezo mahususi kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuelekea tamasha la kihistoria la kuhamasisha Sensa kupitia Sanaa na Michezo (Sensabika).
Akizungumza na Vyombo vya Habari leo Agosti 15, 2022 jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya kilele cha kampeni ya (sensabika) kuhamashisha sensa Agosti 21, 2022 katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam amesisitiza kuwa kuanzia sasa BASATA wanatakuwa kutumika kuhamasisha kila program ya Serikali kupitia Sanaa na Michezo.
Amesema Sanaa na Michezo ni nguvu laini ( soft power) ambayo ina nguvu kubwa katika kuhamasisha maendeleo ya nchi.
Amesema maadhimisho ya kilele cha tamasha hilo la kistoria yamekamilika na ametoa wito kwa wananchi note nchini kuhudhuria.
Ameongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbalimbali na sanaa mbalimbali za maonesho ikiwa ni pamoja na jogging.
Amesema mbali na ni michezo ya hapa nyumbani pia mchezo wa yoga utachezwa kwa kuongozwa na kampuni ya Arts of Living.
Katika hatua nyingine Dkt. Abbasi ametumia jukwaa hilo kuelezea mafanikio makubwa yaliyojitokeza kutokana na Royal Tour.
Ameyataja mafanikio ya ujumla kuwa Royal tour imefungua milango ya kila sekta duniani.
Katika mkutano huo Dkt. Abbasi aliambatana na viongozi wakuu wa mashirikisho na mabaraza ya michezo ambao walipata fursa ya kuchangia kwa ufupi ushiriki wa wadau wao kwenye tamasha