Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Mbeya

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana emesema umefika wakati kwa Tanzania kuwa na barabara nne kila upande kutoka Dar es Salaam hadi Tunduma kwa ajili ya kufungua fursa zaidi za kiuchumi.

Ametoa kauli hiyo leo Julai 29,2022 wakati akizungumza kwenye kikao cha wanachama CCM wa Mkoa wa Mbeya alipokuwa akielezea uamuzi wa Serikali kujenga barabara nne katika Jiji la Mbeya.

“Kazi iliyobakia ni kuharakisha mkandarasi apatikane lakini sio kupatikana bali apatikane na ujenzi uanze haraka ili tutakapofika 2025 tuwe na barabara nne, lakini jana wakati nasafiri kutoka Tunduma kuja Mbeya.

“Mawazo yangu yananielekeza hivi sasa Tanzania umefika wakati wa kuwa na barabara nne kutoka Dar es Salaam mpaka Tunduma.Tusifanye vipande vipande ndugu wabunge.

“Sijui una kipande cha kilomita 10 unafikiri ndio umetatua tatizo,ikitengenezwa barabara nne nne katika kilometa 10 zile kilometa zikiisha unarudi tena kwenye barabara moja,” amefafanua Kinana.

Hivyo amesema ni wakati wa umefika kuwa na barabara nne nne kila upnde kwasababu itakuwa imesaidia kukuza uchumi na kutoka Bandari ya Dar es Salaam mpaka Tunduma hebu angalia yale malori unayokutana nayo kila siku.

“Kama tungekuwa na barabara nne upande huu nne na upande huu nne ni barabara zitakazodumu katika miaka 50 ijayo, ni barabara zitakazokuza uchumi wa mikoa yote Dar es salaam ,Pwani Morogoro, Iringa , Mbeya,Songwe Tunduma mpaka Zambia na magari yataongezeka , fedha zitaongezeka,kwa hiyo umasiki utapungua.

Katika hatua ngingine, Kinana amesema amepokea ombi la wananchi wa Mkoa wa Mbeya kutaka eneo la Tanganyika Packers ambalo kwa sasa limekuwa pori, hivyo wanaomba waruhusiwe kuliendeleza kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

“Kuhusu eneo la Tanganyika packers mimi ninavyojua haya ni maeneo yalichukuwa wakati wa Mwalimu Julius Nyerere,yalichukuliwa kwa ajili ya kujengwa maeneo ya machinjio ya kisasa,lengo lilikuwa nzuri.

“Moja lilijengwa hapa(Mbeya) na lingine likajengwa Shinyanga lakini kwa miaka ya zaidi 40 machinjio hakuna, shughuli hazipo, eneo limekaa bure na wananchi wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo wakati mawazo wanayo na mipango wanayo .

“Mimi mwenyewe niwahakikishie wana CCM na wana Mbeya wenzangu kesho nitafikisha ombo hili kwa Rais Samia Suluhu Hassan,”amesema Kinana wakati akijibu ombi la Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera kwa niaba ya wananchi wa mkoa huo,” amesema.

Kuhusu ombi la wananchi wa Mkoa wa Mbeya kutaka ndege kubwa ziwe zinatua usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe ambao hivi sasa umewekewa taa ,Kinana amesema ombi hilo tayari amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kuangalia kama inawezekana