Baba ambaye anadaiwa kutaka kuwauza watoto wake watatu albino alikamatwa nchini Msumbiji wakati wakijadiliana kuhusu bei, Polisi wamesema.

Mwanamume huyo (39) na kaka yake (34), walikamatwa katika Jimbo la Tete Magharibi.Wamekanusha shtaka hilo, kwa mujibu wa Polisi.

Watu wenye ualbino wameuawa nchini humo kwa ajili ya viungo vyao vya mwili vinavyotumika kwa matambiko.

Msemaji wa Polisi Feliciano da Câmara amesema wanunuzi wawili pia wako chini ya ulinzi wa Polisi.

Amesema watoto hao watatu wenye umri wa kati ya miaka 9 na 16 walichukuliwa kutoka nyumbani kwao na kuzuiliwa huku mazungumzo ya bei yao yakiendelea.

“Uuzaji huo ulipaswa kufanywa kwa zaidi ya $39,100 (£32,400),’’ msemaji huyo wa Polisi amesema.

“Tulichukua hatua na kuwapata watu hao wawili huko Angónia ambao walithibitisha mipango ya mpango huo,’’ ameongeza.