Mifano ya ujasiriamali yenye uthubutu lakini ikakwamishwa
Mwaka 2004 hadi Mei 2006 nilikuwa nimetumia uwezo wangu wa masoko kusajili dawa ya kiasili ya Dental Formula Power (DFP), ambayo inasaidia kutibu na kukinga meno yasipate magonjwa na kuzuia wazee wabaki na meno yao kinywani yakiwa imara hadi wanaingia kaburini.
Basi nikatumia ushawishi kwenye mamlaka za nchi nyingine na Dental Formula Power (DFP) ikawa dawa ya kwanza kusajiliwa katika nchi nyingine na kuruhusiwa kuuzwa kwenye jamii (public) kupitia maduka ya dawa, supermarkets na katika hospitali zao, wakati ikiwa ni dawa ya miti shamba na ambayo haijatengenezwa kisasa.
Kwa uhakika ni kwamba tangu nimezindua hiyo DFP na kuisajili kwenye nchi za Kenya, Uganda, Zambia na Malawi mpaka hivi leo, kuanzia mwaka ule wa 2004/2005 nilipozisajili kwa mara ya kwanza huko, imeweka historia kuwa ni dawa ya kwanza na bado mpaka hivi leo hakuna dawa nyingine ya kiasili ambayo haijaendelezwa, yaani ikiwa katika mfumo wa kusagwa tu (crude) kama DFP ambayo iliwahi kupata kibali kwa kusajiliwa rasmi na mamlaka za dawa na kuruhusiwa kuuzwa katika maduka ya dawa na hospitali za nchi hizo.
Sasa badala ya kumpa sifa Mtanzania huyu na kumuunga mkono, maadui zangu wanajenga fitina kunilaza Psychiatric kwa mara nyingine tena, ili niwe nalala tu, nisiwe na uwezo kabisa wa kuwaza na kufanya chochote huku wakiendelea kushawishi umma kuwa mimi ni mgonjwa wa akili.
Kwa hiyo ndugu zangu kama nilivyosema awali, sasa si wakati wa kuendelea kujificha kuwa mimi ni nani hasa. Mimi ni mmoja wa watu wenye upeo mkubwa wa kimaono katika kuona fursa na uwezo wa kujua ni njia gani inafaa kufanikisha fursa husika (mimi ni Great Thinker au Visionary).
Wala siwezi kujificha tena kwani nikiwa ‘visionary’ wa taifa na dunia, Mei mwaka 2006 nikawa nimefanya mikakati yote ya kuzindua dawa ya DFP kwa wakati mmoja katika nchi zote nne. Nilifanya mikataba na vyombo vya habari vya Tanzania, Uganda, Kenya na Zambia na kulipa pesa nyingi sana za matangazo hayo ya promosheni. Mradi mzima ulitugharimu mwaka huo wa 2006 karibu Sh bilioni 1.3 taslimu.
Kwa hiyo jambo la kushangaza, baada ya kuanza matangazo katika nchi zote nne kwa wakati mmoja; kama baada ya siku 10 za kuanza promosheni hiyo kubwa ambapo katika nchi hizo zote nilikuwa nimepata vibali vya usajili na matangazo, kwa Tanzania baada ya kukataliwa kibali na TFDA mwaka 2004, niliomba kibali kwa katibu mkuu ambapo nilishukuru Mungu kwani alinipatia kibali cha kuuza na kutangaza DFP. Sasa TFDA hiyo hiyo iliyokataa kunipa kibali mwaka 2004, baada ya siku 10 tu ya kuanza promosheni ya mabilioni katika nchi nne kwa miaka hiyo ya 2006, nikiwa Kampala nilipigiwa simu na ofisi yangu hapa Tanzania kuwa DFP imepigwa marufuku na TFDA.
Wakati huo kulikuwa hakuna Whatsapp ningetumiwa wakati uleule hiyo marufuku. Kwa hiyo promosheni ikasitishwa wakati huo huo katika nchi zote nne. Sasa fikiria hasara ambayo nilipata nikiwa mzawa mwenye uthubutu. Na fikiria taifa lilikosa mapato kiasi gani na ajira ngapi kama hiyo fursa ingeendelea hadi hivi leo.
Lakini badala ya kuhamaki, kuugua, kukasirika au presha kupanda, haikutokea hata kidogo; waliokuwa karibu yangu waliniona nikitabasamu na kuwaambia nchi yangu inanisikitisha, kwani badala ya kunisaidia ndiyo inanirudisha nyuma. Hata watu wengi walinishauri niwashitaki TFDA wanilipe fidia, lakini nikaona TFDA ingekuwa sawa na kumshitaki mzazi, nikasamehe.
Na kwa hakika ni kwamba wakati huo nilikuwa bado kijana ambaye damu ilikuwa bado inachemka, nilikuwa na kasi ya ajabu sana. Kwani mwaka 2004 baada ya maonyesho ya Sabasaba ndani ya juma moja tu nilifungua ofisi katika mikoa 10 ya Tanzania na nikaweka fenicha na juma lililofuata nikawatuma vijana wawili wawili kila mkoa ili kuzifungua ofisi na kuanza kuuza dawa. Na ndani ya wiki mbili baada ya Sabasaba ya mwaka 2004 nikapata mawakala karibu 120 wa nchi nzima.
Kwa hiyo mnaweza kuona watu wa vipaji maalumu si watu wa kuua au kupoteza, ni watu wenye nguvu, uthubutu wa kutoogopa kujaribu wala hasara. Kwa hiyo serikali zetu kama zingekuwa zinawaona na kuwatia moyo, hakika ingekuwa ni kama umewachochea moto wa petroli si mafuta ya taa katika kuleta kasi ya maendeleo.
Kwa kuona ushuhuda (testimonies) pamoja na vipindi mbalimbali ambavyo tumefanya kwa ajili ya dawa na dawa zetu, tafadhali tembelea website yetu.
Kwa mara ya pili, mwaka 2010 nikawekeza kwenye teknolojia za usalama wa vyombo vya mawasiliano yaani simu, kompyuta, laptop na teknolojia hizi za sim-banking ambapo ndiye nilikuwa mtu wa kwanza kwa wakati huo kuziingiza nchini, Afrika Mashariki na kusini ukiondoa Afrika Kusini. Na hawa washirika wangu wa teknolojia baada ya kuona uwezo wangu wa masoko tukasaini mkataba wa miaka mitano kama nikimaliza kuzindua teknolojia zao Afrika Mashariki na kusini wangenipa Bara zima la Afrika.
Nikapeleka wataalamu nje ya nchi kutoka hapa nchini ili wakajifunze hizo teknolojia na wakati wa uzinduzi ambao ulifanyika kuanzia Machi Mosi, 2010, nilileta mtaalamu kutoka nje kuwasaidia wataalamu wangu hapa nchini.
Tulikuwa tumefundisha vijana wa IT karibu 150 ambao tuliwasambaza nchi nzima ili kuhudumia watu wa mikoani na nilipanga ‘floor’ nzima ya PPF Tower, ghorofa ya 17. Uwekezaji mzima kwa mwaka huo wa 2010 ulikuwa karibu Sh bilioni 1.6, hapo baadhi ya pesa nilikuwa nimekopa kwenye kampuni za microfinances ambazo kwa wakati huo walikuwa wakitoza riba asilimia 20 kwa kila mwezi kwa pesa ambazo wamekukopesha.
Maana kwa wakati huo kupata mikopo kutoka benki za wananchi ilikuwa si kazi nyepesi hasa kwa miradi ambayo ilikuwa mipya nchini kama ya kwangu ya kuhusu teknolojia mpya, kwa hiyo benki walikataa.
Mkasa wa tatu wa kukwamishwa
Baada ya kukaa kikao kati yetu wadau wa tiba asili na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Baraza la Tiba Asili, Desemba 2015; Waziri wa Afya akatuhakikishia kuwa kuanzia kikao kile hakutakuwa tena na marufuku katika kutangaza huduma zetu. Kwa hiyo kwetu watu wa maono tukasema huu ndiyo wakati uliokubalika, nikaamua kwa nguvu zote kuwa sasa ndiyo wakati wa kuwekeza kwa nguvu zangu zote kwenye dawa asili.
Tangu nilipozindua dawa ya kwanza ya DFP mwaka 2004, niliongeza dawa nne tu zikawa dawa tano mwaka 2007. Nikawa naogopa kuwekeza zaidi, kwa kuogopa kupigwa marufuku kwa matangazo ya dawa asili na tunakuwa tunapata hasara.
Basi, tukafanya mikakati ya kuzindua ‘fomula’ mpya za dawa 45, lakini mpaka maonyesho yanaanza Sabasaba ya 2016, tulifanikiwa kuzindua ‘fomula’ 34 mpya na tukawa na dawa jumla ya 39. Mradi mzima na uzinduzi wa hizo dawa mpya uligharimu Sh milioni 850.
Tulizindua dawa hizo mpya Sabasaba kuanzia Julai Mosi hadi 10. Tulipomaliza uzinduzi huo tarehe 10, tukawa tunajiandaa kufanya matangazo na promosheni ya nchi nzima. Pigo ni kwamba siku mbili tu baada ya uzinduzi, yaani tarehe 12/07/2016, Baraza la Tiba Asili; wakapiga marufuku matangazo na promosheni.
Ukizingatia biashara wakati huo ilikwishaanza kudorora, tukafilisika vibaya mno kwa sababu dawa zote za mamilioni tulizotengeneza ziliishia kuharibika. Kwa hiyo mradi ukafa, tukajitahidi kulipa mikopo, tukafika mahali tukashindwa kulipa; kwa hiyo tukafilisiwa mali zetu. Tangu uzinduzi huo wa dawa na hasara tuliyopata mpaka hivi leo hatujanyanyuka, bali tumefilisika.
Baada ya kutembea milangoni mwa wafanyabiashara wakubwa, taasisi za fedha na viongozi wa kitaifa kuomba usaidizi wa kupatiwa mitaji na kushindikana; ndiyo maana leo nimekuja kwenu (NGUVU YA UMMA) ili kwa moyo wa hiari na kulingana na uwezo wako unikomboe. Nauita mpango huu ni mzuri na fursa ya kipekee kwa sababu mtaji wako utakaoingiza leo, utarudishwa kwako kwa asilimia 100 baada ya miezi 12.
Kwa hiyo fedha ambazo utatuchangia tutazitumia kufanya promosheni ya dawa ya meno ya DFP katika nchi za Tanzania, Kenya na Malawi ambapo dawa yetu ya DFP imesajiliwa hadi sasa. Na hapo tukipata pesa tutazindua kampeni ya kusajili dawa hii ya DFP katika nchi zote za Afrika. Kwa hiyo kampeni hii ya promosheni ya dawa ya DFP kwa nchi za Kiafrika, ndiyo itatupatia mtaji wa kuendesha miradi mikubwa ambayo nimeifafanua awali.
Nimepata uteuzi wa dunia kuongoza WBVC
Ni kwamba nimependekezwa kuwa Mwenyekiti wa Muunganiko wa Watu Maalumu Wenye Maono Makubwa (Blessed visionaries) duniani, yaani tunaitwa: “Worldwide Blessed Visionaries Community (WBVC)” ambapo Makao Makuu ya WBVC yatakuwa Tanzania au Marekani na muunganiko huu na ofisi kuu vitazinduliwa mwaka 2022 na kila nchi kutakuwa na tawi la WBVC kwa ajili ya kusimamia masilahi ya wanachama. Na wamependekeza Kampuni yetu ya JKBRS International Co. Ltd itakuwa mwenyeji wa muungano huo kwa Bara la Afrika, kwa ajili ya kusimamia miradi maalumu ya kusaidia Bara la Afrika ambayo kwa umoja wetu tutaianzisha kwa kutumia pesa za kampuni na watu ambao wamekwisha kufanikiwa kiuchumi duniani.
Huu ni mchakato ambao tayari umeanza na utachukua muda kukamilika, kwa sababu utahusisha kupata baraka za mamlaka na siasa tofauti za nchi mbalimbali. Lakini miradi hii itakapoanza ambayo itakuwa ikisimamiwa moja kwa moja na wanamaono waliobarikiwa, utakuwa ni ukombozi wa Bara letu la Afrika.
Tanzania itakuwa mnufaikaji mkubwa kwa sababu ‘Billing Centre’ ya miradi yote itakuwa hapa nchini (nitaorodhesha baadaye miradi ambayo tayari tumeimependekeza kwa ajili ya Bara la Afrika baada ya uzinduzi wa WBVC mwaka 2022). Wakati taratibu zote zitakapokamilika, wafadhili wa miradi yote kwa Bara la Afrika tayari wamekwishajitokeza na watajitokeza wengi. Kwa sababu wafadhili wakubwa ni wanachama wenyewe wa WBVC, ambao tayari wamefanikiwa kiuchumi duniani, wakiwa na biashara kubwa.
Wengi wenu mnaweza kuwa mnajiuliza inawezekanaje kwangu kupendekezwa, kuwa mwenyekiti wa WBVC wakati bado si tajiri kama wanachama wengine? Kama ukiangalia wasifu (biography) kwenye waraka huu na kama utatembelea website yangu ya www.jkbtanzania.co.tz au ukaingiza ‘link’ hizi kwenye simu yako: https://www.jkbtanzania.co.tz/revelation-profile, utapata kuona miradi ambayo niliiandika ikiwa ni maono ya kutumia teknolojia zilizovumbuliwa na wavumbuzi waliobarikiwa (devoted innovators) ili kujenga, kuboresha na kuendeleza maisha na mazingira ya dunia na wanadamu wanaoishi sawa. Kwa hiyo wana maono wenzangu kwa kuyapitia maono hayo ya miradi ya kusaidia wanadamu, wakakubali kwa kauli moja kuwa hiyo miradi inaweza kutekelezeka ili kusaidia dunia.
Na kutokana na hilo, ndiyo maana wameniteua mimi kuwa mwenyekiti, wakijua nitawaongoza kikamilifu kufikia kwenye malengo hayo, wakati kwa sasa nilianguka kimtaji kutokana na miradi yangu kufilisiwa kwa uamuzi wa makosa kutoka katika taasisi za serikali yangu.
Ndiyo maana ninakuja kwenu wananchi wenzangu ili mwenye kidogo au kikubwa anichangie kwa hiari, ili kuficha aibu hii, iwapo si mchango wa bure, utapata mrabaha mkubwa sana wa maisha. Huko nje wanachama wenzangu wa WBVC wanajua kuwa na mimi nina uwezo wa kifedha mkubwa wakiangalia miradi mbalimbali kwenye mitandao ambayo nimefanya.
Na pia, wamenipa uenyekiti kwa sababu wao ni ‘visionaries’, hawana mioyo ya unafiki wala hila, wameona hayo maono ya miradi ni Mungu amenifunulia kwa faida ya wanadamu wote duniani, si kwa hasara, bali faida; ndiyo maana wakafuata mfano wa Farao wa nyakati za Yosefu (Joseph) mwana wa Yakobo katika maandiko ya Mungu.
Ukisoma andiko la kuanzia Mwanzo 41:39-43 ni baada ya Mungu kumfunulia Yosefu maana ya ile ndoto ya Farao juu ya ng’ombe saba na masuke saba yaliyokonda na ng’ombe saba na masuke saba yaliyonona; ndipo Farao alitoa uamuzi na maagizo yafuatayo na kielelezo hicho cha Farao, ndicho kigezo kilichofanya wanamaono wenzangu wasio kuwa na hila, fitina au wivu wanichague kuwa mwenyekiti wao wakiamini Mungu atanifunulia maono zaidi juu ya kutimiza miradi hiyo kuliko mtu mwingine miongoni mwao ambaye ana elimu ya kidunia tu na utajiri kuliko mimi. Soma hapa maneno yafuatayo kuhusu uamuzi wa Farao kwa Joseph wa kipindi hicho: “Kisha Farao akamwambia Yosefu: Kwa kuwa Mungu amekuwezesha kuyajua yote hayo, hakuna mtu mwenye busara na mwenye hekima kama wewe. 40 Wewe binafsi utaisimamia nyumba yangu, na watu wangu wote watakutii kabisa. Mimi nitakuwa mkuu kuliko wewe katika kiti cha ufalme tu.” 41 Tena Farao akamwambia Yosefu: “Ona, nakuweka juu ya nchi yote ya Misri.” 42 Kisha Farao akaivua pete yake rasmi ya muhuri kutoka mkononi mwake, akaiweka mkononi mwa Yosefu na kumvalisha mavazi ya kitani bora, naye akaweka mkufu wa dhahabu shingoni mwake. 43 Tena akampandisha katika gari la pili la heshima alilokuwa nalo, hata wapaaze sauti mbele yake, “Avrekh!” hivyo akamweka juu ya kila kitu katika nchi ya Misri.”
Kwa hiyo wana maono wenzangu wameridhia kuwa kuna kitu cha ziada ambacho Mungu amenipa kuliko wao, ni bora wanipe uongozi wa umoja wetu WBVC. Lakini nchi yangu inaniona mimi ni kichaa, iwapo nimeshafanya miradi mikubwa sana bila kupata msaada wa taasisi au kiongozi yeyote.
Bali ninapoizindua miradi hiyo kwa gharama kubwa sana, ndani ya siku 10 wanaipiga marufuku bila kuniuliza chochote, ili nitoe ufafanuzi wa miradi hiyo nilivyoianzisha na nilifuata sheria gani na ambapo wajiridhisha kuwa kuna kasoro ndipo waipige marufuku.
Lakini wewe unaamka asubuhi unashangaa umeletewa barua ya kupigwa marufuku mradi mkubwa na wenye manufaa kwa taifa na ajira nyingi za Watanzania; kwa hiyo kama wangeniachia nyakati hizo na kunisaidia kuiendeleza miradi hiyo, bila shaka kwa leo ingekuwa miradi mikubwa sana Afrika na msingesikia nazunguka kwa matajiri na taasisi za fedha na leo nakuja kwenu wananchi eti kuomba mtaji.
Kwa sasa nina mradi mwingine mkubwa ambao tumeingia makubaliano na shirika moja la kidini lenye makao yake makuu nchini Marekani ambalo lina wanachama na familia zao wanaokaribia watu milioni 20 duniani, wameonyesha nia ya wanachama wao duniani kutumia dawa zetu nne ambazo ni virutubisho yaani dawa ya LIFE, DFP, JOY na S-one. Na hawa wanachama wao watakuwa wakiuza virutubisho hivi vinne vikiwa sehemu ya kipato chao (source of income) yao kupitia mauzo ya moja kwa moja (direct selling) kwenye maeneo yao duniani.
Kwa hiyo makadirio (projection) ya miaka sita ijayo itakuwa ni sisi na wao, tutashirikiana ili kujenga uwezo wa kuzalisha virutubisho hivyo vinne kwa ajili ya ya kuweza kuhudumia watu wasiopungua watu milioni 120 duniani kwa kila mwezi. Kwa sababu hizi ‘supplements’ zingine unapaswa kuzitumia kila mwezi na zingine kila baada ya miezi mitatu na sita; matarajio ni kuingizia taifa karibu Sh bilioni 500 kila mwezi.
Ndiyo maana nina uhakika wa kuwalipa wananchi watakaonichangia mtaji leo, mrabaha wa asilimia 100 kila mwezi kulingana na kiasi atakachochanga leo, kwa wale watakaofanikiwa kunichangia hadi kufikia siku ya Jumapili ya tarehe 21/07/2019 na asilimia 20 watakaonichangia kuanzia tarehe 22/07/2019 na mrabaha hautakuwa wa mwezi mmoja au mwaka bali kila mwezi na kwa maisha mtu na warithi wake wanne.
Kwa hiyo mtu mwenye maono na uthubutu wa kuona fursa na asiyeogopa hasara (risk) namkaribisha aniunge mkono nipate mtaji wa kunyanyukia hapa nilipokwama (taking off) na wewe upate msingi wa maisha ya uhakika kiuchumi kwa maisha yako yote.
Pamoja na kwamba tuna mradi mkubwa wa mabilioni kila mwezi, lakini kuna masharti ya kufanya kabla ya kuanza biashara rasmi mwaka 2022, ambapo tutaanza na wanachama wao wanaokaribia milioni tatu wa Afrika Mashariki na Kusini.
Masharti ni kwamba tunapaswa kufanya utafiti kamili wa kisayansi na majaribio ya kliniki kwa kila dawa, pili utafiti wa ardhi inayofaa kwa kulima mimea ya dawa hizo katika ardhi ya Tanzania, Kongo (DRC) na Uganda na kujenga kiwanda ambacho kitakidhi uzalishaji dawa salama (GMP) na kiwanda kikiwa na uwezo wa kuzalisha dawa za awamu ya kwanza kwa watu milioni tatu kuanzia mwaka 2022.
Naishukuru serikali yangu pendwa imeanza mchakato wa kunitafutia mtaji kwa ajili ya kuanzishia huu mradi mkubwa. Kwa hiyo michango kutoka kwako, serikali na mauzo ya DFP katika nchi ambazo tutafanikiwa kuisajili na kuizindua, yatatupatia pesa za kutosha kwa ajili ya kutimiza masharti ya kuzindua mradi wa kwanza wa dawa nne kwa ajili ya dunia.
Kwa maelezo zaidi nipigie: 0767 700 900.
Tembelea tovuti ya Gazeti la JAMHURI, www.jamhurimedia.co.tz ili kusoma sehemu ya kwanza ya makala hii iliyochapishwa wiki iliyopita.