TIMU ya Taifa ya Ufaransa imefanikiwa kunyakua Ubingwa wa Dunia mwaka 2018 baada ya kuifunga Croatia kwa bao 4-2.
Mabao ya Ufaransa yamewekwa kimiani na Mario Mandzukic aliyejifunga, Antoine Griezmann aliyefunga kwa njia ya penati pamoja, Paul Pobga pamoja na Kylian Mpabbe.
Wakati huo mabao ya Croatia yamepachikwa kimiani na Ivan Perisic pamoja na Mario Mandzukic aliyesahihisha makosa yake kwa kuifungia timu yake bao la pili.
Ubingwa huo kwa Ufaransa unakuwa wa pili baada ya kuutwaa pia katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1998 nchini kwao.
Kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps amekuwa miongoni mwa makocha watatu kutwaa ubingwa huo kama mchezaji na Kocha baada ya Mbrazil Mario Zagallo na Mjerumani Franz Beckenbauer.
Vilevile Ufaransa imekuwa timu ya kwanza kufunga mabao manne katika fainali hizo tangu Brazil iifunge Italia 4-1 mwaka 1970.